KIONGOZI wa wapiganaji wa kundi la M23 Mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo ametangaza kuwa watasitisha mapigano katika vita vyao na Jeshi la Serikali. Bertrand Bisimwa alisema kwenye taarifa yake kwamba anawasihi wapiganaji wote kusitisha mapigano na wanajeshi, ili kuwezesha kuanza kwa mazungumzo ya amani. Hata hivyo wakati kauli hiyo ya M23 ikitolewa wanajeshi wa serikali, wakisaidiwa na kikosi …
Kiongozi wa Taliban Auawa Nchini Pakistan
SHAMBULIZI la ndege ya Marekani inayoruka bila rubani limefanikiwa kumuuwa kiongozi wa Taliban, Hakimullah Mehsud nchini Pakistan. Mehsud alitwaa madaraka baada ya mtangulizi wake kuuawa mwaka 2009. Kifo hicho ni pigo kubwa kwa kundi hilo na kimetokea baada ya serikali kusema imeanzisha mazungumzo ya amani na wanamgambo wa kundi hilo. Mehsud alikuwa kwenye orodha ya wahalifu wanaosakwa na Marekani huku …
Basi ‘Laigonga’ Treni Kenya, 12 Wafariki Dunia
WATU 12 wamefariki dunia baada ya treni ya abiria kuligonga basi lililokuwa likivuka reli jijini Nairobi, Kenya. Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema watu wengine waliokuwa kwenye basi hilo pia wamejeruhiwa kufuatia ajali hiyo mbaya. Ajali za barabarani zinazosababisha idadi kubwa ya vifo hutokea kila mara nchini Kenya. Kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria za barabara na mabasi yanayojaa abiria …
Prof Kaimenyi Ataka Kubadilishana Matokeo ya Utafiti
Na Anne Kiruku, EANA, Arusha WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Kenya, Profesa Jacob Kaimenyi amewataka washiriki wa mkutano wa mwaka huu wa Jukwaa la Wasomi na Sekta Binafsi kubadilishana uzoefu wa utafiti waliojifunza, hususan na watengenezaji sera. Prof. Kaimenyi alikuwa anazungumza katika chakula cha jioni kilichoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika hoteli moja mjini Nairobi, …
Serikali ya Kabila Kumzika Tena Mobutu Sese Seko Nchini Congo
SERIKALI ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, imesema itahamisha mabaki ya mwili wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mobutu Sese Seko kufuatia makubaliano na familia yake. Kwa mujibu wa taarifa ya Rais wa nchi hiyo, Joseph Kabila serikali imedhamiria kufanya hivyo ikiwa ni juhudi za kujenga uhusiano mzuri kwa wanakongo. Hayati Mobutu alizikwa nchini Morocco, alikofariki mnamo mwaka 1997 baada …