Price Charles Afungua Mkutano wa Jumuiya ya Madola Sri Lanka

Na Anna Nkinda – Colombo, Sri Lanka MKUTANO wa 22 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola umefunguliwa leo mjini Colombo nchini Sri Lanka kwa mara ya kwanza na mtoto wa Malkia wa Uingereza, Price Charles bila ya kuhudhuriwa na Malkia Eizabeth wa Pili ambaye ni Mkuu wa Jumuiya hiyo. Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Mahinda …

Kongo Yaitupia Lawama Uganda Baada ya Mazungumzo ya Suluu Kuvunjika

UJUMBE wa serikali ya Kongo umejiondoa katika mazungumzo na waasi wa M23 yanayosimamiwa na Uganda, baada ya pande hizo mbili kutofautiana kuhusu vipengele vya muafaka wa amani uliolenga kumaliza uasi nchini Kongo. Msemaji wa serikali wa Kongo, Lambert Mende amesema Uganda imechangia kuvunjika kwa mazungumzo hayo. “Uganda inaonekana kuchangia kama sehemu ya mgogoro huo. Inaegemea upande wa M23,” alisema Mende. …

Walioathiriwa na Kimbunga Waitaji Msaada Uphilipino

SIKU nne baada ya Kimbunga Haiyan kupiga katika Mji wa Tacloban, nchini Uphilipino, maelfu ya watu bado wanaitaji msaada wa dharura. Umoja wa Mataifa (UN) umetoa wito kwa jamii ya kimataifa kutoa msaada wa dola millioni 301 ili kuwasaidia watu nchini Ufilipino. Wakitoa ombi hilo mjini Geneva, wafanyikazi wa UN wamesema masuala yanayopewa kipaumbele ni chakula, maji na dawa licha …

10,000 People are Believed Dead in Philippine…!

TACLOBAN, Philippines (AP) – As many as 10,000 people are believed dead in one Philippine city alone after one of the worst storms ever recorded unleashed ferocious winds and giant waves that washed away homes and schools. Corpses hung from tree branches and were scattered along sidewalks and among flattened buildings, while looters raided grocery stores and gas stations in …

Mkutano wa Amani na Usalama EAC Kufanyika Nchini Burundi

Na Mwandishi wa EANA, Arusha MKUTANO wa pili wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) kuhusu masuala ya Amani na Usalama utafanyika mjini Bujumbura,Burundi kati ya Novemba 13 na 15, mwaka huu. “Mkutano huo utatoa fursa ya majadiliano kuhusu juhudi za kujenga amani, kuzuia migogoro na ufumbuzi na pia kubadilishana uzoefu wa aina hiyo kutoka jamii nyingine,” alisema Charles Njorege, Naibu …

Waandishi wa Habari Watekwa na Kuuwawa, Miili Yao Yatupwa..!

IMERIPOTIWA kuwa watu wenye silaha wamewateka nyara na kuwauwa waandishi wa habari wawili wa redio moja ya nchini Ufaransa ambao walikuwa wakielekea Kaskazini mwa Mali kwa shughuli za kikazi Novemba 02, 2013. Maofisa wa nchi za Ufaransa na Mali walisema watu hao wenye silaha waliwakamata waandishi hao wakati walipokuwa wakitoka katika nyumba ya kiongozi wa waasi. Vifo hivyo vinakuja siku …