Mtalii wa Denmark Abakwa Nchini India

POLISI nchini India wanachunguza kisa cha mtalii wa kike raia wa Denmark aliyebakwa na genge la watu mjini Delhi. Taarifa zinasema mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 51 alikuwa amepotea njia wakati akirejea hotelini alikokuwa anaishi katikati mwa Mji wa Delhi. Taarifa zaidi za Polisi zinasema mtalii huyo aliporwa kwa mabavu na kisha kubakwa akishikiwa kisu. Tayari mwanamke huyo ameondoka …

Mazungumzo ya Sudan Kusini Yakwama Kuanza

MATUMAINI ya kupatikana kwa amani nchini Sudan Kusini yameingia mashakani baada ya mazungumzo ya ana kwa ana ya pande zinazopingana yaliyokuwa yakitarajiwa kufanyika nchini Ethiopia kuchelewa. Waziri wa Mambo ya nje wa Ethiopia, Tedros Adhanom amesema mazungumzo hayo yaliyokuwa yafanyike siku ya Jumamosi hayatafanyika kama ilivyokuwa imetarajiwa. Alisema mikutano inaendelea mjini Addis Ababa ili kuandaa agenda za mazungumzo hayo ya …

Kamanda wa Al Qaeda Afariki Dunia Akiwa Kizuizini

MAJESHI ya Lebanon yametangaza kuwa kamanda wa cheo cha juu wa kundi la kigaidi la Al Qaeda katika nchi hiyo Majid Al – Majid amekufa akiwa kizuizini. Kamanda huyo ambaye ni raia wa Saudi Arabia, alikuwa kiongozi wa kundi la Abdulha Azzam ambalo lina uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda, ambalo pia limekuwa likikiri kuendesha mashambulizi ya kigaidi …

Brotherhood Wakichoma Moto Chuo Kikuu cha Misri

WANAFUNZI ambao ni wanachuo na wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood lililopigwa marufuku nchini Misri wamepigana na polisi kwenye Chuo kikuu cha Al Azhar mjini Cairo na kuchoma baadhi ya majengo ya chuo hicho. Taarifa zinasema katika vurugu hizo mwanafunzi mmoja ameuawa. Maofisa usalama wanasema wanafunzi hao walijaribu kuwazuia wenzao wasifanye mitihani na baadaye kuchoma moto kitivo cha biashara wakati …

Viongozi wa IGAD Wajadili Mgogoro wa Sudan Kusini

VIONGOZI wa Afrika Novemba 27, 2013 wanazungumzia mzozo unaozidi kukuwa Sudan Kusini wakati Umoja wa Mataifa ukiharakisha uingizaji wa vikosi zaidi nchini humo kukomesha umwagaji damu katika taifa hilo changa kabisa. Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya walikutana na Rais Salva Kiir mjini Juba na kufanya mazungumzo ya kutafuta suluhu na wamekiri mambo yanaendelea. …

Vita Wenyewe kwa Wenyewe Vyanyemelea Sudan Kusini

JESHI la Sudan Kusini limesema linajiandaa kufanya shambulio kubwa dhidi ya vikosi vya waasi wakati nchi hiyo inayoelekea kuingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe licha ya juhudi za kimataifa za kutafuta suluhu. Uwezekano wa kuzuka kwa mapigano makubwa umekuja wakati Umoja wa Mataifa ikionya kwamba hali katika taifa hilo jipya hilo changa kabisa duniani inatibuka kwa haraka ambapo hivi …