AU Yaunda Jeshi Maalum Kuzinusuru Sudan Kusini na Afrika ya Kati

NCHI wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) zimetangaza kutuma kikosi maalumu cha wanajeshi watakaoshughulikia mizozo kwa dharura ili kumaliza umwagaji damu katika nchi mbili za Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati barani humo zilizokumbwa na mizozo. Mwenyekiti mpya wa umoja wa Afrika na ambaye ni Rais wa Mauritania Mohammed Ould Abdel Aziz alisema wameamua kuundwa kwa kikosi hicho …

Obama Aapa Kuizunguka Congress

RAIS wa Marekani, Barack Obama ameapa kulizunguka bunge na kuchukua hatua kivyake ili kuwaimarisha watu wa tabaka la kati, akionyesha kukatishwa kwake tamaa na kasi ndogo ya kutunga sheria kwa upande wa bunge hilo. Katika ujumbe wake kwa Bunge la Congress kupitia hotuba yake ya kila mwaka kwa taifa, Obama aliahidi kuchukua hatua kukabiliana na ongezeko la ukosefu wa usawa, …

Majengo ya Polisi, Usalama Yashambuliwa Cairo

ZAIDI ya watu wanne wameuwawa na wengi kujeruhiwa kufuatia mashambulio matatu ya mabomu karibu na vituo vya polisi katika Mji Mkuu wa Misri Cairo. Shambulio la kwanza lilitokea eneo la uwanja yanakoegeshwa magari ambalo ni Makao Makuu ya Polisi mjini Cairo, katika mlipuko huo mtu mmoja anadaiwa kujilipua akiwa ndani ya gari eneo hilo. Kwa mujibu wa duru za idara …

Serikali na Waasi Sudan Kusini Wasaini Kusitisha Mapigano

SERIKALI na waasi wa Sudan Kusini wamesaini makubaliano ya kusitisha mapigano, japokuwa wachambuzi wa mambo wanasema bado kuna kazi kubwa ya kuwadhibiti wapiganaji na kutekelezwa kwa makubaliano ya mkataba huo. Makubaliano hayo yaliyosainiwa Mjini Addis Ababa, Ethiopia, Januari 23, 2014 na pande zote za mzozo kwa kukubaliana kumaliza mapigano yaliodumu takribani kwa wiki tano ambayo yamesababisha vifo vya maelfu ya …

UN Yaizuia Iran Kushiriki Mkutano wa Kusaka Aman Syria

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon amesitisha mwaliko wa kutaka nchi ya Iran kushiriki mazungumzo ya kutafuta suluhu kati ya pande zinazozozana nchini Syria. UN imefikia uamuzi huo baada ya Iran kutupilia mbali mashariti yaliyokuwa yakiambatanishwa na mwaliko huo wa kushiriki mazungumzo. Msemaji wa UN, Martin Nesirky alisema Ban Ki-moon ameubatilisha mwaliko wa Iran baada ya nchi …

Mtafaruku Mazungumzo ya Amani Syria, Upinzani Wawakataa Iran Kushiriki

MAZUNGUMZO ya amani nchini Syria ambayo yanatarajiwa kufanyika baadaye wiki hii yamekumbwa na sintofahamu, baada ya Umoja wa Mataifa (UN) kuialika Iran kushiriki katika mazungumzo huku upande wa upinzani ukitishia kuyasusia kutokana na mwaliko huo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameialika Iran kwenye mazungumzo ya Montreux. Mwaliko huo kwa Iran umetangazwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa …