WAKAZI wa kijiji kimoja Magharibi mwa Sri Lanka wameshangazwa na pia kwa namna nyingine kufurahishwa na tukio la ‘kunyesha’ kwa mvua ya Samaki wadogo kijijini kwao. Samaki hao ambao walikuwa katika hali nzuri ya kuweza kulika wanaaminika kuwa walibebwa kutoka kwenye mto mmoja kwa upepo mkali na kuangukia kijijini hapo. Wanakijiji hao wa Wilaya ya Chilaw walisema walisikia kitu kizito …
Wadau Anuwai Wakutana Kuijadili Elimu EAC
Na Mtuwa Salira, EANA-Arusha WASOMI wabobevu, watawala, watafiti na waandaaji sera wanakutana mjini Arusha, Tanzania kuanzia Mei 5, 2014 kubadilishana uzoefu juu ya changamoto zinazoikabili sekta ya elimu na mfumo wake katika kanda ya Afrika Mashariki. Mkutano wa tatu wa Taasisi ya Ubora wa Elimu ya Juu Afrika Mashariki (EAQAN) utafanyikia katika hoteli ya kitalii ya Ngurdoto, nje kidogo ya …
John Kerry Awasili Sudani Kusini Kusaka Amani
John Kerry awasili Sudan Kusini WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, ametaka kusitishwa kwa mapigano yanayoendelea Sudan Kusini ili kuepusha kutokea mauaji ya kimbari. Kerry ametoa kauli hiyo wakati alipowasili mjini Juba, Sudan Kusini jana. Ziara hiyo ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani inaonekana kuwa ni hatua mojawapo ya kumaliza mapigano yanayoendelea kati ya wanajeshi …
Sudani Kusini Kujadiliwa EAC Oktoba
Na Ronald Ndungi, EANA, Arusha MAJADILIANO juu ya ombi la Sudani Kusini kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yameahirishwa hadi Oktoba mwaka huu, Mkutano wa wakuu wa nchi EAC ulisema Jumatano. Mwenyekiti wa Mkutano huo, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alisema mjini hapa kwamba kucheleweshwa huko kutatoa nafasi kwa Sudani Kusini kufanya maandalizi ya kitaifa na mashauriano. “Hata …
Marais EAC Kukutana Jumatano Mkoani Arusha
Na Mtuwa Salira, EANA, Arusha MARAIS wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) watafanya mkutano maalum mjini hapa Jumatano wiki hii, linaripoti Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki (EAN). Mkutano huo wa siku moja utatathmini shughuli za wanachama wa jumuiya hiyo ya kiuchumi katika kanda hii. Miongoni mwa mambo yatakayopewa kipaumbele katika mkutano huo ni pamoja na …
UN Yatafakari Vikwazo Sudan Kusini
BARAZA la Usalama la Umoja wa Mataifa linafikiria kuweka vikwazo dhidi ya makundi yanayopigana nchini Sudan Kusini, huku rais wa nchi hiyo Salva Kiir, akimfukuza kazi mkuu wa majeshi, baada ya waasi kuutwa mji wa Bentiu. Mkuu wa shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa, Herve Ladsous na msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya …