MABINGWA watetezi wa Kombe la Dunia, Hispania wameondolewa kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2014, inayoendelea nchini Brazil baada ya kuchalazwa mabao 2 kwa mtungi na timu ya taifa la Chile. Matokeo ya jana yamewaaibisha mabingwa hao watetezi baada ya kutoka mapema kwenye mashindano hayo tena bila pointi yoyote katika kundi lao ‘B’. Hispania inaungana na timu ya Cameroon …
Al Shabaab Washambulia Kenya, Wauwa Raia 48 Lamu
WATU wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Kiislamu wameshambulia kituo cha polisi, hoteli na vijiji mjini Mpeketoni, pwani ya nchini ya Kenya. Makabiliano makali yameripotiwa kutokea sehemu kubwa ya Jumapili usiku huku wakazi wa maeneo hayo wakikimbilia maeneo ya msitu karibu na kisiwa cha Lamu. Shirika la msalaba mwekundu linasema mpaka sasa watu 48 wanahofiwa kuuawa katika shambulizi hilo lililotokea nyakati za …
Wapiganaji Waislamu Wateka Mikoa Iraq
WAPIGANAJI wa Kiislamu wanadaiwa kuendelea na kuteka maeneo zaidi nchini Iraq, katika hatua ambayo Marekani imetaja kama ni tishio kwa eneo zima. Polisi wa Iraq wanasema kwamba muungano wa makundi hayo – Islamic State of Iraq na Levant – ambao wanajiita kwa pamoja ISIS wameteka mikoa ya Kirkuk na Salehddin. Inasemakana watu nusu milioni tayari wametoroka Mosul, eneo ambalo lilitekwa …
Dk Bilal Ahudhuria Hafla ya Kukabidhiwa Madaraka Prof. Arthur Mutharika
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal leo Jumatatu Juni 02, 2014 ameshiriki katika sherehe za kukabidhi madaraka kwa Rais mpya wa Malawi Profesa Arthur Peter Mutharika katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Kamuzu Banda jijini Blantyre. Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Rais wa Botswana sambamba na wawakilishi wa nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Afrika …
Ban Ki Moon Ampongeza Rais Kikwete
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesifu jitihada za Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mchango wake mkubwa katika kupigania Afya ya Mama na Mtoto. Bw. Ban Ki Moon ametoa pongezi Mei 30, 2014 wakati alipokuwa akizungumzia juhudi za kumuokoa Mama na Mtoto baada ya Mwaka 2015, mwishoni mwa mkutano wa siku 3 kuhusu Afya ya Mama na Mtoto kama ilivoainishwa …
Moto Uliozuka Hospitalini Wauwa Wagonjwa 21
WAGONJWA wapatao 20 pamoja na muuguzi wameuawawa baada ya moto mkubwa kuibuka hospitalini katika Jimbo la Janseong nchini Korea Kusini. Moto huo pia umewaacha wagonjwa wengine 6 wakiwa mahututi baada ya moto huo katika hospitali ya Hyosarang iliyoko kilomita 300 kusini mwa Seoul. Wengi waliofariki dunia kwa ajali hiyo ya moto ni wagonjwa wazee wenye umri kati ya miaka 70 …