WANAMGAMBO wa Al Shabaab wamedai kuwa wamemuua kwa kumfyatulia risasi mbunge maarufu mjini Mogadishu. Taarifa zinasema, Ahmed Mohamud Hayd (Mb) aliuawa baada ya kutoka hotelini ambapo katika tukio hilo, mlinzi wake pia aliuawa huku Katibu wa Bunge akibaki amejeruhiwa. Kundi la Al-Shabaab, ambalo lina uhusiano na lile la al-Qaeda, limeapa kuendelea na mashambulizi zaidi katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu …
Waislamu Waadhimisha Ramadhan
WAISLAMU wanaokadiriwa kufikia bilioni 1.6 duniani Jumapili wameanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan ambapo huacha kula na kunywa kwa kutwa nzima na kuepuka kila aina ya maovu kabla ya kula majira ya jioni. Hata hivyo mwezi mtukufu umegubikwa na machafuko ambayo hayakuwahi kushuhudiwa kabla ya umwagaji damu na uhasama wa madhehebu wenye kutishia kuisambaratisha Mashariki ya Kati ambacho ni …
Tanzania Yaongoza Mkutano wa Kamati ya Viongozi Afrika Kuhusu Tabia Nchi
Na Premi Kibanga, Malabo-Equatorial Guinea NCHI za Afrika zinatakiwa kuwa na msimamo mmoja kuhusu jinsi ya kukabiliana na madhara ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa barani Afrika. Misimamo huo wa Afrika unatarajiwa kuwasilishwa kwenye mkutano mkubwa wa Dunia kuhusu masuala ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa unaotarajiwa kufanyika New York, Marekani Mwezi Septemba, 2014. Akiwakilisha ripoti ya Kamati ya Viongozi …
Bara la Afrika Latakiwa Kupunguza Madhara ya Hali ya Hewa
KUTOKANA na kiwango kilichofikiwa cha Tabia Nchi hivi sasa, nchi za Afrika hazina budi kuungana na kuchukua hatua za kupunguza madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa kwa pamoja. Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo Juni 25, 2014 Mjini Malabo, Equatorial Guinea wakati akifungua Mkutano wa Wakuu wa Nchi 11 zinazounda Kamati ya Mazingira ya Nchi za Umoja wa Afrika …
Serikali Yamchunguza Aliyepewa Zawadi ya Mke Kijijini
TUME inayohusika na masuala ya usawa wa kijinsia nchini Afrika Kusini inafanya uchunguzi kuhusu madai kuwa Mkuu wa Shirika la Habari la SABC nchini humo alikabidhiwa msichana mwenye umri wa miaka 23 kama zawadi awe mkewe. Tume hiyo imesema kuwa imepokea malalamiko kwamba viongozi wa kitamaduni walimkabidhi Mkuu Shirika la Habari la Serikali SABC, Hlaudi Motsoeneng mke kama zawadi jambo …
Uganda Yasema Haitishwi na Vikwazo vya Marekani Kuhusu Ushoga
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Uganda, Balozi James Mugume, amesema kuwa Uganda haitishwi na vikwazo ilivyowekewa na Marekani kama hatua ya kupinga sheria yake kali kuhusu mapenzi ya jinsia moja. Balozi Mugume alisema kuwa Serikali ya Uganda itafanya mazungumzo na Marekani ili kufafanua hatua waliyochukua. Alisisitiza kuwa wataieleza Marekani sheria hiyo inapinga tabia ambayo sio ya …