TIMU ya Taifa ya Ujerumani imetwaa kombe la dunia. Ujerumani imetwaa kombe hilo jana baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Argetina 1-0. Mchezaji wa Ujerumani, Mario Goetze ndiye aliyeiwezesha Ujerumani kutawazwa mabingwa wapya wa kombe la dunia. Mchezaji Goetze aliizamisha Argetina katika dakika za nyiongeza baada ya timu hizo kucheza dakika 90 za kawaida bila kufungana na kucheza tena …
UN Yataka Mapigano Yasitishwe Gaza
BARAZA la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) limetaka mapigano baina ya Israel na Wapalestina yakome katika Ukanda wa Gaza, na kuanza kwa mazungumzo ya amani kutafuta suluhisho la amani ya kudumu. Tangazo hilo lililoungwa mkono na wanachama wote 15 wa baraza hilo limezitaka pande hizo mbili kurejea katika makubaliano ya kusitisha uhasama ya Novemba, 2012 ambayo yalisimamiwa na Misri, …
Israel Yazidisha Mashambulizi Gaza
WATOTO watano wa Kipalestina ni miongoni mwa watu 21 waliouwawa katika mashambulizi ya angani yanayofanywa na Israel katika ukanda wa Gaza, hii ni kulingana na wataalamu wa afya katika ukanda huo. Vifo hivyo vimeongeza idadi ya watu waliouwawa kufikia 80 tangu Israel ilipoanzisha mashambulizi ya angani siku ya Jumanne, dhidi ya Ukanda wa Gaza. Akizungumza na wanahabari Msemaji wa Huduma …
Wandishi wa Al Jazeera Wafungwa Miaka 7, Rais wa Misri Apinga…!
MAHAKAMA nchini Misri imewahukumu kwenda jela kwa kifungo cha kati ya miaka saba na kumi wandishi watatu wa habari wa Shirika la Habari la Al Jazeera waliokuwa wamezuiliwa kwa miezi sita nchini humo. Taarifa zinasema waandishi hao walipatikana na hatia ya kueneza habari za kupotosha na kushirikiana na kundi la wapiganaji wa Kiisilamu la Muslim Brotherhood. Mmoja wa wandishi hao, …
Wakenya Zaidi 20 Wauwawa Mkoa wa Pwani
TAKRIBANI watu 21 wameuwawa katika mashambulizi kwenye kaunti mbili za mwambao wa Kenya, ambapo Jeshi la Polisi Kenya limewalaumu wanaharakati wanaotaka kujitenga katika Mkoa wa Pwani kuhusika na mashambulio hayo. Naibu Mkuu wa Polisi Kenya, Grace Kaindi alisema watu 21 wameuwawa katika mashambulizi hayo mawili ya usiku na kuwalaumu wanachama wa Chama cha Mombasa Republican Council (MRC) kundi lenye kupigania …
Watanzania Waitikisa Marekani kwa Utapeli
BAADHI ya Watanzania wanaoishi Marekani huenda wakaozea jela baada ya kutiwa hatiani na wengine kukiri mahakamani kuhusika katika utapeli na wizi wa mamilioni ya Dola za Marekani, kupitia mikopo na upangishaji wa nyumba. Hukumu ya hivi karibuni ni ya Mtanzania, Mokorya Cosmas Wambura (41) ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela na faini zaidi ya Dola 400,000 (zaidi ya Sh660 …