Hatimaye Dawa na Kinga ya Ukimwi Vyagundulika

WATAFITI katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Temple, Marekani wamegundua dawa ya kuangamiza Virusi Vya Ukimwi (VVU) ambayo ni ya uhakika zaidi ukilinganisha na zilizowahi kupatikana katika tafiti za awali duniani. Dawa yao inaweza kutumika kwa tiba ya wanaoishi na VVU na kinga kwa wale ambao bado hawajaambukizwa. Mmoja wa watafiti hao, Dk Kamel Khalili aliwaambia waandishi wa …

Sekta ya Uzalishajia Bidhaa Yadoda EAC

Na Anne Kiruku (EANA) ROBO tu ya bidhaa zinazouzwa nje ya Kanda ya Afrika Mashariki zinatokana na sekta ya uzalishaji zikiwemo bidihaa za vyakula, vinywaji, ngozi na mazao ya ngozi. Taarifa iliyotolewa mwishoni mwa wiki jijini Nairobi imebainisha kuwa sekta hiyo ina uwezo mkubwa wa kutengeneza ajira zaidi ili kukabiliano na tatizo sugu la ukosefu wa ajira katika kanda ya …

Tamasha la Waafrika Ujerumani Lafunika!

Tamasha hili linafikia tamati leo tarehe 20/7/2014, baada ya kuanza tarehe 17/7/2014. Tamasha hili hufanyika kila mwaka hapa jijini Tuebingen, Ujerumani, ambapo waafrika hutumia fursa hii kuonyesha utamaduni wao kupitia bidhaa mbalimbali, ikiwemo miziki.     Picha na habari: dev.kisakuzi.com, Tuebingen, Ujerumani    

Ndege ya Malaysia Yaanguka, Yaua Abiria 295

NDEGE ya Shirika la Ndege Nchini Malaysian ikiwa na abiria 295 imeanguka Mashariki mwa Ukraine ikiwa safarini kutoka Amsterdam, Uholanzi kuelekea Kuala Lumpur na kuua abiria wote. Taarifa za awali zinasema ndege hiyo imedunguliwa ikiwa angani. Taariza zaidi zinasema miili ya watu imetapakaa kila upande karibu na Kijiji cha Grabovo, eneo ambalo linadhibitiwa na waasi wanaotaka kujitenga. Ndege hiyo aina …

Mtuhumiwa wa Ugaidi Kenya Akamatwa Tanzania

MMOJA wa watuhumiwa wa matukio ya ugaidi nchini Kenya, Jihad Gaibon Swaleh, amefikishwa mahakamani nchini Tanzania kwa tuhuma hizo. Mshukiwa huyo amesomewa mashtaka ya kufadhili vitendo vya kigaidi nchini Kenya. Watuhumiwa wengine 16 ambao wanadaiwa kuendesha vitendo vya kigaidi nchini Tanzania pia wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na tuhuma za kula njama ya kutenda makosa ya kigaidi nchini Tanzania. Washtakiwa wote 17 …