George Bush Ampongeza Mama Salma Kikwete

Na Anna Nkinda – Maelezo, Washington RAIS wa zamani wa Marekani George W. Bush amempongeza Mke wa Rais Mama Kikwete kutokana na kazi nzuri anayoifanya ya kuhamasisha jamii na wanawake kujitokeza kwa ajili ya kupima saratani ya matiti na mlango wa kizazi. Pongezi hizo zilitolewa jana na Rais huyo mstaafu ambaye pia ni mwanzilishi wa Taasisi ya George W. Bush …

Rais Kikwete Asema Umeme Kikwazo cha Maendeleo Afrika

Na Mwandishi Maalum, Washington, D.C. RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa moja ya sababu kubwa zinazokwamisha maendeleo makubwa na ya haraka zaidi ya Afrika ni uzalishaji mdogo na matumizi ya chini mno ya umeme. Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa hali hiyo inaeleza jinsi ongezeko la uzalishaji na matumizi ya umeme linavyoweza kuharakisha maendeleo ya …

EAC Yaonguza Kupunguza Migogoro katika Nchi zake

Na James Gashumba, EANA Nchi tatu za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) za Rwanda, Burundi na Tanzania zimetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi zilizofanikiwa kuharakisha kwa kasi kubwa kukua kwa maendeleo endelevu ya binadamu kwa kupunguza migogoro na kujenga ushupavu baina ya raia wake kati ya mwaka 2000 na 2013. Taarifa ya hivi karibuni iliyotolewa na Shirika la Mpango wa …

Kijiji Chafunikwa na Udongo, Watu 20 Wafariki

ZAIDI ya watu 200 wanahofiwa kukwama katika maporomoko ya udongo nchini India, huku 20 wakithibitika kufariki dunia katika Kijiji cha Malin karibu na Mji wa Pune lilikotokea janga hilo. Kazi ya uokoaji inaendelea katika eneo hilo huku hali ya hewa mbaya ikidaiwa kuchelewesha harakati hizo. Vikosi vya uokoaji vimeendelea na kazi ya kuwanusuru waliofukiwa na maporomoko ya udogo, japo kuwa …

Liberia Yaomba Kusaidiwa Kukabiliana na Ebola

WAZIRI wa Habari nchini Liberia, Lewis Brown ameomba msaada nchi yake kusaidiwa kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola unaolikabili taifa hilo. Amesema Liberia inahitaji msaada toka Jumuiya za Kimataifa ikiwa ni pamoja na kutumiwa wataalam wa tiba ili wasaidie kidhibiti ugonjwa huo. Waziri huyo ameuelezea mlipuko wa ugonjwa huo kuwa si wa kawaida hivyo wanaomba kusaidiwa. “Huu bado …