WATU 80 wameuawa na wengine zaidi ya mia tatu kujeruhiwa, baada ya bomu lililotegwa kwenye gari kulipuka mjini Kabul. Maafisa nchini humo wanasema mlipuko mkubwa ambao umetokea katika eneo la makazi ya wanadiplomasia mapema asubuhi. Wingu la moshi mkubwa lilikuwa limetanda na kuonekana katika maeneo mengi ya mji wa Kabul. Aidha nyumba zilizokuwa jirani na bomu hilo lilipolipuka pia zilipatwa …
Marekani Yajaribu Mfumo Wake wa Utenguaji Makombora
NCHI ya Marekani kwa mara ya kwanza imefanikiwa kufanya majaribio kwenye mfumo wake wa kudungua makombora ya masafa marefu ‘ICBM’ hii ikiwa ni kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maofisa wake. Mfumo huo wa ardhini uliwekwa katika kambi moja ya kijeshi mjini California na kudungua kombora la masafa marefu kulingana na kitengo cha ulinzi wa makombora MDA. Taarifa zaidi …
Rais wa Marekani Trump Akiwa Ziarani Nchini Israel
RAIS wa Marekani Donald Trump amewasili nchini Israel akiendelea na ziara yake ya kikazi katika maeneo ya Mashariki ya Kati ambapo pia anatarajiwa kuzuru Maeneo ya Wapalestina. Amefika huko akitokea Saudi Arabia, mshirika muhimu wa Marekani, ambako alitoa hotuba katika mkutano mkuu wa nchi za Kiarabu na Kiislamu. Bw Trump anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa Israel na …
Ndege Vita za China Zaizuia Ndege ya Marekani
NDEGE mbili za kijeshi za China zimeizuia ‘vibaya’ ndege ya Marekani kulingana na jeshi la Marekani. Ndege hiyo inayohusika na kufanya uchunguzi, ilikuwa katika safari yake ya kutaka kugundua mionzi katika anga ya kimataifa iliopo mashariki mwa bahari ya China. Ndege hiyo ilikuwa imetumiwa kugundua ushahidi kuhusu majaribio ya kinyuklia ya Korea Kaskazini. China imekuwa ikituhumu vitendo vya Marekani …
Rais Donald Trump Aipa Tanzania Dola Milioni 526
SERIKALI ya Marekani kupitia ofisi ya rais Donald Trump imetangaza kupatia Tanzania ufadhili wa kukabilana na virisu vya ukimwi. Marekani, ambayo siku chache zilizopita ilitangaza kusimamisha ufadhili wake kwa wizara ya afya nchini Kenya, imeipa Tanzania kitita cha dola milioni 526. Kitita hicho kutoka mfuko wa PEPFAR, kitatumika kufanikisha mpango wa kutoa huduma kwa zaidi ya watu milioni 1.2 wanaoishi …
Trump Aunga Mkono Mpango wa Nyuklia wa Iran
IKULU ya Whitehouse nchini Marekani imeendeleza mpango wa kuipunguzia vikwazo Iran licha ya rais Donald Trump kuukosa mpango huo. Kuondolewa kwa vikwazo ni miongoni mwa makubaliano ya kinyuklia yalioafikiwa 2015 chini ya aliyekuwa rais Barrack Obama pamoja na mataifa mengine matano yenye uwezo mkubwa duniani. Bwana Trump ameelezea makubaliano hayo kuwa mabaya zaidi. Hatahivyo wizara ya fedha nchini humo iliwawekea …