Papa Francis Aanza Ziara Yake Sri Lanka, Waasi FDLR…!

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Farncis amewasili nchini Sri Lanka kwa ziara ambako anatarajiwa kusisitiza umhimu wa mazungumzo baina ya makundi mbalimbali ya imani hasimu za kidini nchini humo. Pamoja na hayo, Papa Francis akiwa nchini humo anatarajiwa kuhimiza suala la maridhiano wakazi walio wengi wa visiwa vya Sinhalese na wale wachache wa kisiwa cha Tamil. Hii ni ziara …

Boko Haram Wateka Kambi ya Jeshi Nigeria, Shahidi wa ICC Afariki

MAOFISA nchini Nigeria wamesema kuwa kundi la Boko Haram limeuteka Mji na kambi moja ya kijeshi inayotumiwa na wanajeshi wa kimataifa wanaojaribu kukabiliana na wapiganaji hao. Seneta wa Borno Kazkazini Maina Ma’aji Lawan, eneo la Mji wa Baga amesema kuwa wanajeshi waliitoroka kambi yao baada ya kushambuliwa na Boko Haram jumamosi asubuhi. Wakaazi wa Baga, ambao walitoroka kupitia maboti hadi …

Boti Yazama na Kuuwa 36, Askari wa UN Wauwawa Somalia

TAARIFA kutoka Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imeeleza kuwa mashua moja iliyokuwa imebeba bidhaa na abiria imezama na karibu watu 36 wamefariki dunia. Maofisa wanasema kuwa zaidi ya watu 100 wamenusurika. Inaripotiwa kuwa ajali hiyo ilitokea siku ya Jumatatu umbali wa kilomita 30 kutoka Mji wa Kisangani na kusababisa maandamano yaliyofanywa na vijana wenye hasira kwenye Mji …

Mbunge Adai Kuvuliwa Nguo Bungeni

KUFUATIA vurugu na purukushani zilizoonekana katika bunge la Kenya wakati wa kupitishwa kwa mswada wa usalama, mbunge mmoja mwanamke sasa amejitokeza na kudai kwamba wabunge wenzake watatu wanaume walijaribu kumvua nguo. Mbunge huyo Millie Odhiambo aliandika katika mtandao wake wa facebook kwamba wabunge wengi walipigwa huku yeye akidai kupigwa ngumi machoni na mbunge mmoja kabla ya wabunge wawili kujaribu kumvua …

Dk Bilal Amwakilisha JK Mkutano wa Kimataifa wa Mazingira Duniani

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal Desemba 09, 2014 amemuwakilisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Mwenyekiti Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali Barani Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi, kwenye mkutano wa Kimataifa wa Mazingira Duniani (Cop20) unaofanyika jijini Lima, Peru.   Pamoja na shughuli nyingine ambazo zimemuhusisha Makamu wa Rais …

JK Afungua Jengo jipya Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumatatu, Desemba 8, 2014, amefungua rasmi Jengo la Shughuli Nyingi (Multipurpose Hall) la Ikulu katika moja ya shughuli zake za kwanza baada ya kuanza rasmi kazi kufuatia upasuaji mwezi uliopita. Sherehe hiyo ya ufunguzi wa Jengo hilo lililoko upande wa kushoto wa Bustani za Ikulu upande wa Lango …