NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), J. Eliasson ameliambia Jopo la Watu Mashuhuri linaloongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kuwa hakuna shaka duniani kuwa magonjwa ya milipuko, kama vile Ebola, yataendelea kuisumbua dunia katika miaka ijayo na hivyo ni lazima maandalizi yafanyike kukabiliana na hali hiyo. Aidha, Naibu Katibu Mkuu huyo amelitaka Jopo …
Vurugu za Ubaguzi Afrika Kusini; Nigeria Yaondoa Mabalozi Wake
TAIFA la Nigeria limewaita mabalozi wake waishio nchini Afrika Kusini kurejee nyumbani kufuatia mashambulizi ya kibaguzi dhidi ya wenyeji yanayofanyika Afrika Kusini. Mpaka sasa watu saba wameshapoteza uhai kufuatia mashambulizi hayo, yaliyoanza wiki tatu zilizo pita. Mali zimeharibiwa vibaya na mashambulizi hayo yamezusha hofu kubwa miongoni mwa raia wa kigeni. Balozi wa Nigeria mjini Pretoria, mji wa kibiashara na kwingineko …
African Space Research Program
Vijana (Wanasayansi) nchini Uganda, wameanzisha African Space Research Program na mpaka sasa wamemaliza project mbili ya kwanza ni military craft, na ya pili ni PROJECT X, hiyo military craft itaanza kufanya kazi watakapopowe ruhusa na serikali ya Uganda. Chanzo http://www.ugandanway.com/
Nchi za Afrika Zaweka Msimamo Dhidi ya IMF na WB
WAKATI Mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la kifedha la kimataifa ikiendelea hapa Mjini Washington Dc. Mawaziri wa fedha wameweka misimamo yao juu ya sera ambazo zinawekwa na Benki ya Dunia. Akizungumza na vyombo vya habari,waziri wa fedha wa Tanzania Mhe. Saada Salum Mkuya alisemaā€¯ Sisi kama nchi tuliwasilisha nini tunaona katika utekelezaji wa mipango ya Benki. Tumeshukuru sana …
Rais Zuma Awatembelea Raia wa Kigeni Wanaoshambuliwa Afrika Kusini
RAIS Jacob Zuma amewatembelea watu walioathirika na ghasia hizo, mauwaji pamoja na kuibwa kwa mali zao huku akiahidi kukabiliana vilivyo na wimbi la mashambulio hayo. Bwana Zuma alifutilia mbali ziara yake nchini Indonesia, ili kukabiliana na vurumai hizo zilizoanza majuma mawili yaliyopita. Amesema kuwa ghasia hizo ni kinyume na maadili ya taifa la Afrika kusini. Maofisa zaidi wa polisi wametumwa …
Shamy Tours and Travel Agent Yatoa Zawadi Mgahawani
Meneja Mwendeshaji wa kampuni ya Shamy Tours and Travel Agent Zanzibar, Bw. Khamis Mwinjuma Simba akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo katika sekta ya utalii Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wakati wa zoezi la kugawa zawadi za vinyago kwa wageni waalikwa zaidi ya 300 waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mgahawa mkubwa unaotoa huduma za chakula cha Kitanzania …