Kiongozi wa Upinzania Auwawa Burundi

KIONGOZI wa chama kidogo cha upinzani nchini Burundi ameuawa kwa kupigwa risasi. Mwili wa kiongozi huyi, Zedi Feruzi pamoja na wa mlinzi wake ulipatikana nje ya nyumba yake kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Bujumbura. Mauaji ya mwanasiasa huyo yanafanyika wakati wanaharakati wa upinzani nchini humo wamesitisha kwa siku mbili maandamano yao dhidi ya Rais Pierre Nkurunziza kupinga uamuzi wake …

Kipindupindu Chawatesa Wakimbizi wa Burundi Tanzania

UMOJA wa mataifa unasema kuwa zaidi ya visa 400 vya ugonja wa kipindupindu vinaripotiwa kila siku miongoni mwa wakimbizi wa Burundi walio nchini Tanzania. Maelfu ya watu wamewasili kwa mashua wakikimbia ghasia za kisiasa nchini Burundi Wamechukua hifadhi katika sehemu zenye misongamano na zilizo na mazingira mabaya. Umoja wa mataifa unasema kuwa takriban watu 3000 wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu na …

Al Shaabab Wavamia Msikiti Kenya, Auwawa kwa Risasi Burundi

VIONGOZI Kaskazini mwa Kenya wamesema wapiganaji wa kundi la kigaidi kutoka Somalia la Al Shaabab wamevamia msikiti mmoja eneo la Garissa kwa masaa kadhaa. Wapiganaji hao waliwahutubia waumini waliokuwa msikitini kwa karibu saa mbili kabla ya kutokomea msituni. Katika hotuba yao waliikosoa serikali ya Kenya na kuonya waumini dhidi ya kuwa majasusi wa serikali ya Kenya. Mwezi uliopita Al Shaabab …

Rais Nkurunziza Awafukuza Kazi Mawaziri Watatu…!

IKIWA ni siku chache baada ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, kunusurika kupinduliwa madarakani amewafukuza kazi mawaziri watatu katika Serikali yake. Hata hivyo bado maandamano ya wananchi yanaendelea katika Mji Mkuu wa Burundi Bujumbura ikiwa ni ishara ya kumshinikiza asigombee muhula wa tatu katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo. Mawaziri walioachishwa kazi ni pamoja na Waziri wa Ulinzi, Waziri wa …

Jeshi Linalomtii Rais Nkurunziza Lazima ‘Mapinduzi’ Burundi

JESHI linalomtii Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza jana lilifanikiwa kuzima mapinduzi ya kijeshi yaliyopangwa kufanywa na wanajeshi wafuasi wa Meja Jenerali Godefroid Niyombare aliyetangaza kupitia kituo kimoja cha redio kuwa ameipindua serikali ya Nkurunzinza. Jeshi linalomtii Rais Nkurunziza limesema tayari limeweka ulinzi katika makazi ya rais na limetoa masaa sita kwa wanajeshi wafuasi wa Meja Jenerali Niyombare wajisalimishe kabla ya …

David Cameron Ashinda Uchaguzi, Mpinzani Wake Ajiuzulu

WAZIRI Mkuu wa Uingereza, David Cameron amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo jana. Chama chake cha Conservative kimepata viti 330 huku kile cha leba kikijipatia 232. Cameron alisema anapania kuendelea kuiongoza Uingereza kwa umoja. Shirika La BBC lilikisia kuwa Cameron na Chama chake angepata ushindi wa maeneo bunge 329. Chama cha Leba kimepata pigo kubwa huko Scotland …