Hatimaye Laurent Gbagbo akamatwa

Laurent Gbagbo akiwa chini ya ulinzi wa majeshi ya Umoja wa Mataifa baada ya kukamatwa kwenye hoteli moja ambamo alikuwa amejificha mjini Abidjan. Taarifa zaidi zinasema vikosi vya wanajeshi vinavyo mtii Alassane Ouatarra vimemkamata kiongozi huyo na sasa yupo chini ya ulinzi na amekabiziwa kwa majeshi ya Ouatarra.

Obama on Libya: ‘We have a responsibility to act’

WASHINGTON – Vigorously defending the first war launched on his watch, President Barack Obama declared Monday night that the United States intervened in Libya to prevent a slaughter of civilians that would have stained the world’s conscience and “been a betrayal of who we are” as Americans. Yet he ruled out targeting Moammar Gadhafi, warning that trying to oust him …

Libya yashambuliwa kutoka kila kona

UINGEREZA, Marekani na Ufaransa zimeyashambulia majeshi ya kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi kutokea angani, majini na nchi kavu katika tukio la kwanza la utekelezaji amri ya Umoja wa Mataifa (UN) ya kuzuia ndege kuruka. Maofisa wa Pentagon, wizara ya ulinzi ya Marekani wanasema Marekani na Uingereza zimevurumisha zaidi ya makombora 110 huku ndege za Ufaransa zikiyashambulia majeshi yanayomtii Gaddafi …

Familia ya Gaddafi yapigwa marufuku Urusi

MOSCOW, Urusi RAIS wa Urusi Dmitry Medvedev juzi alisaini amri ya kumpiga marufuku kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi kuingia au kusafiri kupitia eneo la Urusi. Amri hiyo pia imewagusa watu wengine 15 wakiwamo watoto wa Gaddafi na maofisa waandamizi walio karibu naye. Aidha fedha, mali na rasilimali za kiuchumi, ambazo familia ya Gaddafi inazimiliki au kuzidhibiti pia zimetaifishwa. Wiki iliyopita, …

Maafa ya Japani hayana kifani

WAKATI Japani, taifa lenye nguvu kubwa kiuchumi duniani likihaha katika harakati za uokoaji, mamia kwa mamia ya miili watu waliokufa kutokana na tetemeko la ardhi imeendelea kupatikana. Idadi ya vifo kutokana na tetemeko kubwa la ardhi la kipimo cha 8.9 nchini Japani inaweza kufikia 10,000 katika mkoa wa Miyagi pekee. Awali polisi ilisema zaidi ya watu 2,000 wamekufa au hawajulikani …

Umoja wa Kiarabu waunga mkono vikwazo Libya

UMOJA wa Nchi za Kiarabu umeunga mkono wazo la kuzuia ndege kuruka katika anga ya Libya, huku waasi wakiendelea kufurushwa kutoka miji waliyokuwa wakiishikilia. Mkutano maalumu uliofanyika mjini hapa umelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) kuweka sera hiyo hadi mgogoro wa sasa utakapomalizika. Uingereza na Ufaransa ziliunga mkono wazo hilo lakini hazikuungwa mkono vya kutosha na Umoja …