Shirika la kutetea haki za binaadam la Amnesty International limeitaka serikali ya Misri kufanya uchunguzi kamili baada ya maofisa wa juu wa kijeshi kukiri kuwa waliwafanyia vipimo vya ubikira, wanawake waliokuwa wakiandamana hivi karibuni. Pamoja na hayo, Amnesty imetaka wote waliohusika kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria kujibu udhalilishaji huo. Tuhuma hizo ambazo zinadaiwa kutokea kwa wanawake waliokuwa wakiandamana baada …
NATO imeshambulia nyumba ya Gaddafi
TAARIFA kutoka katika Jeshi la NATO zinaeleza vikosi vya jeshi hilo vimeangamiza minara ya walinzi katika eneo la nyumba ya Kanali Muammar Gaddafi wa Libya mjini Tripoli.Imeelezwa kwamba yamefanyika mashambulio mawili yaliyofanywa na ndege za umoja huo wa kijeshi. Waandishi wa habari mjini Tripoli, wanasema shambulio moja lilofanywa mchana, lilivunja sehemu za ukuta unaozunguka jengo la jeshi la Bab al-Aziziya. …
KIJANA ATUMIA FARASI KUEPUKA BEI KALI ZA MAFUTA MAREKANI!
Na Rungwe Jr. California, CA Juma hili Kamera ya dev.kisakuzi.com ilikuwa maeneo ya Lompoc, California, na kubahatika kukutana na kijana aliyefahamika kwa jina moja la Derek, akiwa na Farasi wake. Kama ilivyo ada, dev.kisakuzi.com ili amua kumuuliza maswali mawili matatu kufahamu kulikoni Farasi yupo kwenye maeneo mbayo ni maegesho ya Magari!? Kijana Derek alinifahamisha kuwa yupo maeneo hayo kumtembelea rafiki yake …
Mali ya Gaddafi yafichuliwa
HATIMAYE eneo kulikofichwa mamilioni ya dola mali ya serikali ya Libya, imebainika. Hii ni baada ya kufichuliwa kwa stakabadhi ya mamlaka ya uwekezaji nchini humo. Stakabadhi maalum ya mamlaka ya uwekezaji nchini Libya, ambayo imeonekana na shirika la kutetea haki za binadamu Global Witness, imeonyesha kwamba hapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka jana takriban dola milioni 293 fedha za umma …
Viongozi G8 kukutana leo Ufaransa
Viongozi wa dunia wanatarajiwa kukutana katika eneo Deauville nchini Ufaransa, kwenye kongamano la mataifa manane yenye utajiri mkubwa zaidi duniani G8. Mkutano wa leo unatokea wakati kumeibuka mataifa mengine ambayo uchumi wake unakua kwa kasi na kuibua hoja ya ushawishi na umuhimu wa G8. Hata hivyo wadadisi wamesema matuko ya hivi karibuni hususan harakati za mageuzi ya kidemokrasia katika nchi …