Mzee Mandela leo tarehe 18/7/2011, ametimiza miaka 93 ya uhai wake! dev.kisakuzi.com inamtakia afya tele na maisha marefu zaidi mzee wetu huyu.
Wafanyikazi wa BBC waanza mgomo
WAANDISHI habari wengi wanaohudumu katika Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) wameanza mgomo wa siku moja kulalamikia mpango wa kuwaachisha kazi baadhi yao. Hii inafuatia hatua ya serikali ya Uingereza kupunguza matumizi yake katika sekta ya umma.Wasimamizi wa BBC wamesema hatua ya kuwapunguza wafanyakazi haingeweza kuepukika. Miongoni mwa idara zilizolengwa ni Idhaa ya dunia pamoja na ile inayofuatilia matangazo kote …
Somalia nchi hatari duniani!
UMOJA wa Mataifa umesema Somalia ni eneo lenye janga kubwa kabisa la kibinaadamu hivi sasa duniani, huku vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano vikiongezeka kwa sababu ya utapiamlo na ukosefu wa usalama. Wakimbizi wa Kisomali wanaokimbia ukame na njaa kwao na kutafuta hifadhi nchini Kenya, wanatajwa kuwa ndio watu mafukara wa mwisho na watu walio kwenye hatari kubwa …
KUZALIWA SUDAN KUSINI: Ni furaha, kilio kwa Afrika?
*Taifa moja lagawanyika katikati ya ndoto za Afrika Moja *Kuendekeza udini, ukabila vyachochea mgawanyiko wake *Kuwa mwanachama mpya Jumuiya ya Afrika Mashariki JUBA, Sudan Kusini MAELFU ya raia wa Sudan Kusini jana walitokwa na machozi waliposhuhudia kupandishwa kwa bendera ya taifa lao jipya katika sherehe za uhuru zilizofanyika katika Jiji la Juba, katika tukio ambalo wachunguzi wa mambo wanasema …
Ajali ya ndege DRC, 50 wahofiwa kufa
DRC, Kongo NDEGE ya abiria iliyokuwa na watu 112 imeanguka kwenye uwanja wa ndege wa Kisangani huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Takriban watu 40 wamekutwa wakiwa hai, lakini wengine zaidi ya 50 wanasemekana kufariki dunia. Ndege hiyo, iliyo chini ya shirika la ndege la Hewa Bora, ilijaribu kutua baada ya hali ya hewa kuwa mbaya ikitokea Kinshasa. Hakuna uthibitisho …
Sudan Kusini sasa nchi huru
Sudan, MAELFU ya Wananchi wa Sudan Kusini wamekusanyika kushuhudia kupandishwa kwa bendera mpya ya nchi hiyo kuashiria kupata uhuru wake, katika mji mkuu Juba. Rais wa Sudan Omar al-Bashir na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ban Ki-moon ni miongoni mwa wageni waliohudhuria shughuli hiyo. Sudan Kusini limekuwa taifa jipya duniani usiku wa kuamkia Jumamosi, lengo ambalo limefikiwa kufuatia mkataba …