Waziri Mkuu Pinda Aibana SADC, Ataka Ijipange Kimikakati

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) haina budi kuweka mkakati utakaohakikisha kuwa nchi wanachama zinakuwa na mpango mahsusi wa kuendeleza viwanda kama ambavyo imekubaliwa kwenye kikao chao kilichomalizika jana. Ametoa kauli hiyo Agosti 18, 2015, wakati akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza mkutano wa 35 wa wakuu wa nchi za …

Rais Salva Kiir Agoma Kusaini Mkataba wa Amani

Rais Salva Kiir Agoma Kusaini Mkataba wa Amani SERIKALI ya Sudan Kusini imekataa kusaini mkataba uliotarajiwa kuleta amani na kumaliza mapigano yaliyodumu nchini humo kwa zaidi ya miezi ishirini. Hata hivyo waasi na makundi ya upinzani wamesaini kwa upande wao, ilhali Rais Salva Kiir ajaridhia kutia saini mkataba huo. Serikali imeomba kuongezewa siku kumi na tano zaidi kushauriana juu ya …

Raia Wafurika Mali Kuona Muujiza Nje ya Ukuta wa Choo

UMATI wa raia umeendelea kufurika eneo moja la Mji Mkuu wa Mali, Bamako ili kujionea kile kilichotajwa kuwa ni muujiza wa kidini kwenye ukuta mmoja ambao umeonekana wiki iliopita. Idadi kuwa ya watu wanaamini picha hiyo nyeupe nje ya ukuta wa choo inamuonesha mtu akisali na kuonekana kama ishara ya ujumbe wa Mungu. Maofisa wa polisi wa kukabiliana na ghasia …

Rais Obama Awatolea Uvivu Viongozi wa Afrika…!

RAIS wa Marekani Barrack Obama, amewapasha viongozi wa Afrika ambao wanaendelea kung’ang’ania madarakani hata baada ya Katiba kutowaruhusu kuendelea kuwania tena nyadhifa zao za urais. Katika hotuba ya kwanza ya Rais wa Marekani kwa muungano wa Afrika katika makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa, amesema kuwa Afrika haitapiga hatua iwapo viongozi wake watakataa kuondoka madarakani baada ya muda …

Madaktari Hospitali ya Wanawake na Watoto Australia Waitamani Tanzania

Na Mwandishi wetu – Canberra, Australia WAFANYAKAZI wa Hospitali ya wanawake na watoto ya Centenary ya mjini Canberra wameonyesha nia ya kufanya kazi nchini Tanzania ili kumuunga mkono Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete katika juhudi zake za kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia afya za wanawake, vijana na watoto wa Hospitali …