Tanzania yapiga marufuku uuzaji wanyamapori

Tanzania imetangaza kupiga marufuku biashara ya kukamata na kuwasafirisha wanyamapori kwenda nje ya nchi. Hatua hiyo imetangazwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akijibu hoja bungeni kuhusu madai kwamba wanyama takriban 130 wakiwemo ndege 16 walitoroshwa kinyume cha sheria mwishoni mwa mwaka jana na kusafirishwa kwenda nchi moja ya Mashariki ya Kati. Katika jibu lake Bw Pinda alisema: “Kwanza tunataka …

Waziri Mkuu wa Uturuki ziarani Somalia

WAZIRI Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan anatarajiwa kuwasili nchini Somalia kuanza rasmi kampeni ya kukabiliana na baa la njaa nchini humo. Waziri huyo katika ziara yake, ataandamana na Waziri wake wa Mashauri ya Nchi za Kigeni pamoja na wake zao. Viongozi hao wamesema wanakwenda nchini Somalia kuonesha wanawaunga mkono raia wa Somalia katika hali ngumu inayolikabili nchi hiyo. Hadi …

Dola milioni 150 zachangwa kuisaidia Somalia

Waziri mkuu wa uturuki Recep Tayyip Erdogan anatarajiwa kuwasili nchini Somalia kuanzisha rasmi kampeni ya kukabiliana na baa la njaa nchini humo. Waziri huyo mkuu ataandamana na waziri wake wa mashauri ya nchi za kigeni na wake zao. Viongozi hao wamesema wako nchini Somalia kuonyesha wanawaunga mkono raia wa Somalia. Raia wa Uturuki wamechanga kiasi cha dola milioni 150 hadi …

Suluhu ya mgogoro wa uchumi Ulaya wapatikana

RAIS wa Ufaransa Nicholas Sarkozy na Chansela wa Ujerumani Angela Merkel wametoa mapendekezo mapya kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi unaokabili mataifa yanayotumia sarafu ya Euro. Viongozi hao wanataka mfumo mpya kusimamia uchumi wa ulaya Baada ya kukutana mjini Paris, viongozi hao walitoa wito wa kile walichokitaja kuwa usimamizi mpya wa kiuchumi na kuyataka mataifa yanayotumia sarafu hiyo kusawazisha bajeti zao. …

Misaada yazidi kumiminika Somalia

    Jumuiya ya nchi za kiislamu imeahidi kutoa msaada wa dola milioni 350 kuwasaidia waathiriwa wa baa la njaa nchini Somalia. Ahadi ya msaada huo ilitolewa baada ya mkutano uliofanyika mjini Istanbul uturuki ambao ulihudhuriwa na Rais wa Somalia Sheikh Sharrif Sheikh Aden. Akizungumza kwenye mkutano huo waziri mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema hatua ya kujitolea kusaidia …

Maelfu waandamana kupinga ufisadi India

Maelfu ya raia wa India wamejitokeza mitaani kumunga mkono mwanaharakati wa kupinga ufisadi Anna Hazare wakiwa na mabango yaliyoikemea na kuishinikiza Serikali imwachie huru. Mwanaharakati huyo,Bw Hazare anashinikiza kufanyika kwa mageuzi katika sheria za kupambana na rushwa na amepanga kuanza kukesha bila kula ili kushinikiza hilo lifanyike. Mwanaharakati huyo mwenye miaka 74, anapinga mswada uliowasilishwa bungeni kwa kuwa waziri mkuu …