Mambo yageuka Tripoli, waasi warudishwa nyuma na Jeshi la Gaddafi

MAPIGANO yanaendelea kati ya pande mbili muhimu Mji Mkuu wa Libya, Tripoli, kwa siku ya tatu mfululizo huku wapiganaji waasi wakipambana na vikosi vinavyomtii Kanali Muammar Gaddafi. Milio ya risasi na milipuko imekuwa ikisikika karibu na hotel inayotumiwa na vikosi vya serikali pamoja na eneo la makazi ya kiongozi wa Libya ya Bab al-Aziziya. Usiku mzima, mtoto wa Kanali Gaddafi, …

Siku za Gaddafi za hesabika

Rais wa Marekani Barack Obama amesema utawala wa Gaddafi umefikia ukingoni na kumtaka aondoke madarakani ili kuepusha damu zaidi kumwagika. Amewataka waasi kuheshimu haki za binadamu, kuonyesha uongozi mzuri, kuhifadhi taasisi za Libya na kuelekea katika demokrasia. Mapigano makali yanaripotiwa kuendelea katika mji mkuu Tripoli, huku utawala wa Gaddafi ukiapa kuulinda mji huo dhidi ya waasi. Waasi nchini Libya wameingia …

Tripoli yachukuliwa na Waasi, mtoto wa Gaddafi akamatwa

PICHA za televisheni zinaonesha Waasi wakiwa katika Uwanja wa Green Square ndani ya Mji Mkuu, huku makundi ya watu wenye furaha wakisherehekea kuwasili kwa waasi hao katika uwanja huo. Taarifa zinaeleza Waasi wamemkamata mtoto wa Gaddafi Saif al-Islam, huku kiongozi mwenyewe akiahidi kuwa ataendelea kupigana. Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Uhalifu wa Kivita, Luis Moreno Ocampo amethibitisha Saif al-Islam, mwanawe …

Majeshi ya NATO yakabidhi ulinzi kwa Afghanistan

Afghanistan imeanza utaratibu wa kuchukua madaraka ya usalama yenyewe, na jimbo la Banyan limekuwa la mwanzo kukabidhiwa na jeshi la NATO kwa polisi wa Afghanistan. Bamiyan, karibu na sanamu ya zamani ya Budha Mawaziri wa Afghanistan na mabalozi wa nchi za nje walihudhuria sherehe hiyo katika jimbo la kati. Mwandishi wa BBC nchini Afghanistan, anasema Bamiyan ni moja kati ya …

Vifo vya askari wa Marekani vyaongezeka Afghanistan

  Askari wa Jeshi la Marekani wameendelea kuteketea na kufikia askari 31 ikilinganisha na mapema miezi iliyopita hii ni kutokana na kuanguka kwa helkopata ya jeshi lao kuanguka.   Wakuu wa Afghanistan wanasema wanajeshi 31 wa Marekani na wanajeshi kadha wa Afghanistan walikufa, wakati helikopta yao ilipoanguka mashariki mwa nchi hiyo. Hiyo ni hasara kubwa kabisa kuifika Marekani katika tukio …

Afghanistan yashambulia ofisi ya Uingereza, Kabul

Washambuliaji waliojitoa mhanga wameshambulia afisi za British Council katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, na kuwaua takriban watu tisa na kushikilia eneo la Ofisi hizo kwa saa kadhaa. Bomu liliotegwa ndani ya gari liliangamiza ukuta unaozingira ua na watu kadhaa waliokua wamebeba silaha nzito wakavamia sehemu za ndani. Baada ya mapambano ya saa kadhaa Balozi wa Uingereza mjini Kabul alisema …