Watu 7 wauwawa Syria, ukandamizaji raia waendelea

WANAHARAKATI wa kutetea haki za binadamu nchini Syria wanasema maofisa wa vikosi vya usalama wamewaua watu saba, akiwemo mwanamke mmoja aliyekufa kutokana na mateso. Watu wanne waliuwawa katika Mji wa Homs katikati ya Syria na waandamanaji wawili wakauwawa katika kitongoji cha Talbisseh, Kaskazini mwa mji huo. Zaidi ya watu 150 wamekamatwa katika saa 24 zilizopita kwenye kitongoji kimoja cha Mji …

Umoja wa Ulaya kuisaidia Libya matibabu

UMOJA wa Ulaya umesema uko tayari kupeleka msaada wa matibabu nchini Libya. Utapeleka mahitaji yanayotakika kwa dharura katika hospitali nchini humo, kuwasaidia raia wengi waliojeruhiwa katika vita. Shirika la misaada la Medicins Sans Frontiers limesema hali katika hospitali za mji mkuu Tripoli inakaribia kuwa balaa, kwa kuwa mahitaji yamepungua mno wakati wa mapigano ya miezi sita. Kamishna wa Umoja wa …

Maofisa wa Polisi Burkina Faso wafungwa

MAOFISA polisi watatu wametiwa gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika kwenye mauaji ya mwanafunzi kutoka Burkina Faso mwezi Februari, na kuchochea ghasia kwa wiki kadhaa. Justin Zongo alifariki dunia baada ya kudhalilishwa akiwa mikononi mwa polisi. Awali serikali ilisema kifo chake kilisababishwa na homa ya manjano, na kusababisha hasira miongoni mwa wengi. Maandamano- yaliyozidi kupamba moto kutokana na …

Joice ataka kifo cha mumewe kichunguzwe

Makamu wa Rais wa Zimbabwe Joice Maimu ametoa wito wa kufanywa uchunguzi wa kifo cha mume wake Solomon kilichotokea wiki iliyopita kwenye shamba lao. Aliyekuwa mkuu wa majeshi, Jenerali Mujuru alikuwa ni mtu mwenye ushawishi mkubwa kwenye chama cha Robert Mugabe cha Zanu-PF. Mwandishi wa BBC alisema kifo chake kimeibua wasiwasi kuwa huenda aliuliwa, na kusababisha mpasuko ndani ya chama …

Kesi dhidi ya Strauss-Kahn yafutwa

JAJI wa Mahakama mjini New York amefuta kesi ya dhuluma za ngono dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Fedha Duniani, Dominique Strauss-Kahn. Hatua hiyo imejiri wakati waendesha mashtaka walitilia shaka uaminifu wa mwanamke anayemshtaki, ambaye ni mhudumu wa hoteli moja, Nafissatou Diallo , mwenye umri wa miaka 32. Bw Strauss-Kahn mwenye umri wa miaka 62, alituhumiwa kumshambulia mwanamke huyo, …

Gaddafi: Aluta Kontinua, nitapambana hadi kifo

KANALI Muammar Gaddafi ameapa kupigana na waasi hadi kifo au ushindi, ripoti zimesema, baada ya waasi kudhibiti makazi yake mjini Tripoli. Televisheni inayomuunga mkono Kanali Gaddafi, al-Urubah, imesema Kanali Gaddafi ambaye bado hajulikani alipo, ametoa hotuba akisema kuondoka kutoka kwa makazi yake kulikuwa ni ”mpango”. Makazi hayo ndiyo yaliyokuwa maeneo ya mwisho chini ya udhibiti wa Kanali Gaddafi mjini Tripoli. …