MKUU wa waasi nchini Libya amesema, Kanali Muammar Gaddafi bado ni tishio nchini humo na duniani kwa ujumla. Mkuu wa Baraza la mpito la taifa (NTC), Mustafa Abdul Jalil amesema majeshi ya umoja wa nchi za kujihami za Ulaya, Nato, na washirika wengine lazima waendelee kuwaunga mkono waasi dhidi ya ‘mtawala wa mabavu.’ Waasi wameudhibiti mji mdogo wa Nofilia wakielekea …
Waasi Libya wakataa mazungumzo
WAPIGANAJI wa Libya wanasema hawataki kufanya majadiliano na Kanali Gaddafi, baada ya pendekezo hilo kutolewa na msemaji wa kanali. Na wapiganaji wa Libya piya wamesema wana wasiwasi juu ya usalama wa watu kama elfu 50, waliokamatwa na jeshi la Kanali Gaddafi katika miezi ya karibuni. Wanafikiri watu hao wamezuwiliwa kwenye mahandaki mjini Tripoli, na wamewaomba watu wanaojua mahandaki hayo yaliko, …
Ndege za Nato zalenga handaki la Gaddafi
WIZARA ya Ulinzi ya Uingereza imesema, ndege za kijeshi za Uingereza zimerusha mabomu kwenye handaki kubwa lililopo Sirte mji alipozaliwa Kanali Muammar Gaddafi. Ndege hizo ziliondoka kutoka kambi ya jeshi iliyopo Nolfolk siku ya Alhamis usiku. Waasi wa Libya nao wanaimarisha majeshi yao kwenye barabara inayoelekea Sirte, wakipeleka vifaru na makombora. Viongozi wa waasi wamezitaka serikali za kigeni kuondoa tanji …
UN yashambuliwa kwa mabomu Nigeria
MWANDISHI wa BBC Bashir Sa’ad Abdullahi ambaye yupo katika eneo la mlipuko amesema ghorofa ya chini ya jengo hilo imeharibika sana. Huduma za dharura zinaondoa miili ya watu kutoka katika jengo hilo huku majeruhi wengine wakipelekwa hospitali, anasema mwandishi wetu. Makundi ya wanamgambo wa Kiislam wamekuwa wakifanya mashambulio katika jiji hilo katika siku za hivi karibuni. Bomu la kutegwa ndani …
Angela Merkel ni mwanamke mwenye nguvu duniani
JARIDA la Forbes limemtaja Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kuwa mwanamke mwenye nguvu kubwa duniani. Jarida hilo limemuelezea Bi. Merkel kuwa kiongozi asiyetiliwa shaka wa Umoja wa Ulaya na ni kiongozi wa uchumi halisi duniani. Waziri wa mambo ya nchi za kigeni wa Marekani, Hillary Clinton, ameorodheshwa wa pili, akifuatiwa na rais wa kwanza mwanamke wa Brazil, Dilma Rousseff, katika …