Mauaji makubwa yafanyika Burundi

TAKRIBANI watu 36 wameuawa baada ya watu wenye silaha wasiojulikana kufyatua risasi kwenye baa iliyojaa watu karibu na Mji Mkuu wa Burundi, Bujumbura, kwa mujibu wa maofisa wa Polisi Burundi. Wamesema idadi ya waliofariki dunia inaweza kuongezeka kwani watu wengi wamejeruhiwa vibaya kwenye uvamizi huo eneo la Gatumba. Kundi la mwisho la waasi la Burundi lilisalimisha silaha zao rasmi mwaka …

Waliolipua mabomu Uganda wahukumiwa

RAIA wawili wa nchini Uganda wamehukumiwa kifungo gerezani kwa kuhusika na mashambulizi ya bomu mwaka 2010 ambayo yalisababisha vifo vya watu 76 katika mji mkuu wa Uganda Kampala. Edris Nsubuga, ambaye amekiri kutega mabomu amehukumiwa miaka 25 gerezani, ihali Muhamoud Mugisha amehukumiwa kifo cha miaka mitano kwa kuhusika katika njama ya kufanya mashambulizi hayo. Wanamgambo wa Kiislamu wa Somalia al-Shabab …

Cameron na Sakorzy waitembelea Libya

Wazirii Mkuu wa Uingereza David Cameron na Rais Sakaorzy wa Ufaransa tayari wamewasili nchini Libya kufanya ziara yao. Viongozi hao wawili ndio wa kwanza kutoka nchi za magharibi, kufika Libya tangu Kanali Muammar Gaddafi kuondolewa madarakani. Nchi hizo mbili ambazo ni wanachama wa shirika la kujihami la Nato ziliongoza operesheni za Nato kukabiliana na vikosi vya Kanali Gaddafi. Wakuu hao …

Watawala wa Libya waomba silaha kujihami!

MKUU wa Baraza la Kitaifa la Mpito nchini Libya, Mustafa Abdul Jalil ameomba vikosi vyake vipewe silaha ili waongeze juhudi zao za kuteka maeneoe mengine ya nchi ambayo yamedhibitiwa na wanaomuunga mkono Muammar Gaddafi. Mustafa Abdul Jalil ameambia BBC kwamba kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani yuko kusini mwa Libya na anapanga kufanya mashambulio. Ujumbe uliondikwa na unasemekana umetoka kwa Gaddafi umeomba …

Ndege yaanguka Angola yaua Majenerali

AJALI ya ndege nchini Angola imesababisha vifo vya watu 26, wakiwemo majenerali wa kijeshi watatu, Ofisa wa Serikali ameiambia BBC. Luis Caetano, Msemaji wa Mamlaka ya Jimbo la Huambo, amesema ndege hiyo ya kijeshi ilianguka baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Huambo. Amesema watu sita wameokoka kwenye ajali hiyo, akiwemo rubani na msaidizi wake. Waandishi wa habari wamesema …

Wakiri kuishambulia Uganda kwa mabomu

WANAUME wawili ambao walishtakiwa kwa kuhusika na ulipuaji wa mabomu mjini Kampala mwaka uliopita wamekiri makosa hayo. Wawili hao ni miongoni mwa washukiwa 14 ambao wanakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo mauaji ya watu 70 katika mashambulio hayo. Washukiwa wa mashambulizi hayo walikuwa 19 lakini watano wakaachiliwa huru jana na Mahakama Kuu mjini Kampala. Wengine miongoni mwao raia wawili wa Tanzania …