Saudia Yakana Uvumi wa Vifo vya Mahujaji

SAUDI Arabia imekana ripoti kuwa mkanyagano uliowaua zaidi ya watu 700 karibu na mji wa Mecca ulisababishwa na kufungwa kwa barabara ili kuruhusu watu mashuhuri kuingia eneo hilo. Wizara ya masuala ya ndani ilisema kuwa madai hayo ni ya uongo na kwamba uvumi huo ulianzishwa na vyombo vya serikali Iran ambayo ilipoteza raia 131. Iran imeilaumu Saudi Arabia kwa mkasa …

Baba Mtakatifu Papa Francis Awasili Nchini Marekani

BABA Mtakatifu Francis jana aliwasili nchini Marekani kuanza ziara ya kwanza kuwahi kuifanya nchini humo maishani mwake. Kwa kawaida marais wa Marekani huwapokea wageni rasmi Ikulu ya nchi hiyo, lakini alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kijeshi wa Andrews ulioko nje kidogo ya jiji la Washington, Baba Mtakatifu alipata heshima ya kulakiwa na Rais Obama na familia yake. Mbali na gwaride la …

Bomu Lalipuka Ikulu Somalia, Lauwa 6

BOMU lililotegwa ndani ya gari limelipuka karibu na lango kuu la jumba la rais katika mji mkuu wa Mogadishu. Takriban watu sita wamefariki, ikiwemo walinzi wa rais.Raia mmoja wa Uturuki pia aliuawa. Hata hivyo watu wengine 10 waliripotiwa kujeruhiwa. Mkutano kuhusu hali ya baadaye ya uchaguzi nchini humo umekuwa ukiendelea katika jumba hilo,lakini ulikuwa umeisha wakati wa mlipuko huo. Wajumbe …

Papa Francis Kuongoza Ibada Havana, Cuba

MAELFU ya waumini wa Kanisa Katoliki wanahudhuria misa mjini Havana ambayo itaongozwa na kiongozi wa kanisa hilo, Papa Francis ambaye anafanya ziara nchini humo kwa mara ya kwanza. Katika ujumbe wake, Papa Francis amezitaka Marekani na Cuba kuendelea kuboresha uhusiano kati yao. Akizungumza kwenye uwanja wa ndege wa Havana anapoanza ziara nchini Cuba na Marekani, papa Francis alipongeza uhusiano ambao …

Mapambano Yazuka Upya Nchini Burkina Faso

MAPAMBANO yamezuka kwenye hoteli moja katika Mji Mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou, ambako mazungumzo ya amani yamekuwa yakifanyika, baada ya mapinduzi ya juma lilopita. Mapambano yamezuka kwenye hoteli katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou, ambako mazungumzo ya amani yamekuwa yakifanyika, baada ya mapinduzi ya juma lilopita. Wafuasi kama 50 wa kikosi cha kumlinda rais, ambacho kiliipindua serikali ya mpito …

Wapiganaji wa IS Walilipua Kanisa Syria

WAPIGANAJI wa dola ya Kiislamu IS, wanadaiwa kulipua Kanisa la kikristu Mji wa Syria wa Palmyra. Kundi la kutetea haki za binadamu nchini Syria limesema kuwa wanamgambo hao wametumia mabomu kulipua hekalu ya kiroma ya Bel. Taarifa zaidi zinasema kuwa uharibifu mkubwa umetokea baadha ya shambulio hilo, ambapo umelibomoa kabisa hekalu hilo. Wiki iliyopita wanamgambo hao wameoneshwa katika video wakilipua …