Nato yafanya mashambulizi mjini Sirte

NDEGE za kivita za NATO zimeshambulia mji wa Sirte, moja ya maeneo ya mwisho yaliyo ngome za Gaddafi, wakati wanajeshi wa serikali ya Libya wakiendelea kuushambulia mji huo. Wanajeshi wa Baraza la Mpito la Taifa la Libya (NTC) wanakabiliwa na upinzani mkali na wamepeleka vifaru kukabiliana na mashambulio ya kuvizia yanayoendeshwa na wapiganaji watiifu kwa Gaddafi. Wanajeshi wa NTC wanadhibiti …

Mauaji yatokea kwenye maandamano Guinea

INAKADIRIWA Waandamanaji watatu wameuwawa Mji Mkuu wa Conakry nchini Guinea, baada ya majeshi ya usalama kuvunja maandamano ya upinzani. Ripoti zinasema majeshi ya usalama yametumia mabomu ya kutoa machozi na marungu dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe mjini humo. Walitawanya maandamano yaliyokuwa yamepangwa na wanaounga mkono waandamanaji dhidi ya namna serikali inavyojiandaa kwa uchaguzi wa wabunge. Raia wa Guinea walipiga …

Kaburi la pamoja lagundulika Libya

KABURI la pamoja la mamia ya watu lagunduliwa mjini Tripoli, Libya. Kaburi la pamoja linaloaminika kuwa na miili 1,270 limegunduliwa katika mji mkuu wa Libya, Tripoli baraza la mpito la nchi hiyo limesema. Mabaki hayo yanadhaniwa kuwa ya wafungwa waliouwawa na maafisa wa usalama mwaka wa 1996 katika gereza la Abu Salim. Uasi dhidi ya Kanali Muammar Gaddafi ulianza kama …

Profesa Wangari Maathai afariki dunia

Nairobi MWANAHARAKATI maarufu na mtunukiwa wa tuzo ya Amani ya Nobel, Profesa Wangari Maathai amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 71. Mwanaharakati huyo mashuhuri wa mazingira na haki za binadamu wa Kenya Prof. Imeelezwa kuwa Wangari Maathai amefariki dunia mjini Nairobi usiku wa kuamkia, Jumatatu kutokana na maradhi ya saratani. Prof. Karanja Njoroge ambaye ni Mkurugenzi wa Green Belt …

Wanawake Saudia waruhusu kupiga kura

WANAWAKE wa Saudi Arabia hivi sasa wanabaguliwa sana, pamoja na kukatazwa kuendesha gari. Mfalme Abdullah bin Abdelaziz alisema wanawake sasa wataweza kupiga kura na piya kugombea viti, na aliongeza kusema kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya kushauriana na viongozi wa kidini. Mfalme wa Saudia Arabia piya alisema kuwa wanawake watakuwa na haki ya kujiunga na Baraza la Shura..baraza la mashauriano …

Wabunge Ujerumani wamgomea Pope Benedict XVI! Watoka bungeni

Heti siasa na dini ni sawa kuchanganya maji na mafuta katika chupa? Wengine wanadai kisa kupingwa kwa kondomu! Kweli Nabii hana utukufu nyumbani kwao !? KIONGOZI wa kidini wa kanisa la Kikatoliki duniani Mtakatifu Pope Benedict xvi (Joseph Ratzinger), amejikuta yupo katika mvutano mkubwa na wanasiasa nchini ujerumani, baadhi wabunge wapatao 100 wametoka nje ya bunge la ujerumani wakati Pope …