MTOTO wa Muammar Gaddafi aliyekuwa Rais wa Libya aliyeondolewa madarakani kwa nguvu za kijeshi, Muttasim Gaddafi ambaye alifanya kazi kama Mshauri Mkuu wa Usalama wa Kitaifa katika serikali ya babake amekamatwa. Ofisa mmoja wa Baraza la Mpito la Kitaifa nchini Libya (NTC) amesema Mutassim amekamatwa mjini Sirte na kupelekwa Benghazi japokuwa ofisa mwingine kutoka NTC amesema habari hizo bado hazijathibitishwa. …
Raia wa Liberia wajitokeza kupiga kura
RAIA wa Liberia jana wameshiriki katika uchaguzi wa pili tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo miaka minane iliopita. Shughuli ya kupiga kura inatarajiwa kuanza asubuhi hii ambapo wagombea kumi na tano wamejitokea kuwania kiti cha urais akiwemo rais wa sasa Ellen Johnson Sirleaf. Bi Sirleaf anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Winston Tubman wa chama cha …
Vifo vyatokea kwenye maandamano ya wakristo Misri
AMRI ya kutotoka nje imetangazwa mjini Cairo kufuatia machafuko yaliyotokea wakati wa maandamano yaliyofanywa na wakristo wa dhehebu la Coptic, nchini Misri. Inakadiriwa kuwa takriban watu 24 wameuawa na wengine zaidi ya mia mbili wamejeruhiwa vibaya katika machafuko mabaya zaidi ya kidini kuwahi kutokea nchini humo. Wakristo hao walikabiliana na wanajeshi waliowalaani kwa kutowalinda dhidi ya mashambulio yanayotekelezwa na baadhi …
Wakenya wanamuaga Wangari Maathai
BIBI Maathai aliwahi kupata tuzo ya amani ya Nobel, na alikuwa maarufu kwa kazi yake ya kutetea wanawake na mazingira. Ibada ya wafu ilifanywa kwenye bustani ya Uhuru Park, Nairobi, ambayo Wangari aliitetea sana wakati serikali ya Rais Moi ilipotaka kuruhusu majumba kujengwa katika bustani hiyo. Maelfu ya watu walifurika katika bustani hiyo, wakiongozwa na kiongozi wa Kenya, Rais Mwai …
Shambulio baya latokea Somalia
TAKRIBAN watu 55 wameuawa na kinachodhaniwa kuwa mlipuko mkubwa uliofanywa na mtu aliyejitoa mhanga karibu na jengo la Serikali kwenye Mji Mkuu wa Somalia, Mogadishu. Walioshuhudia wamesema lori lililokuwa na milipuko lilikwenda moja kwa moja kwenye lango karibu na wizara moja ya Serikali na kulipua. Sheikh Ali Mohamed Rage, msemaji wa kundi la wanamgambo la al-Shabab, aliiambia BBC kuwa wamehusika …
Mtalii mwingine atekwa Kenya
MTALII mmoja mwanamke wa nchini Ufaransa ametekwa na kundi la watu waliokuwa na silaha karibu na mji wa Lamu, nchini Kenya. Tukio hilo limetokea majuma matatu tu baada ya watalii wawili kutoka Uingereza kushambuliwa piya huko Kiwayu, kaskazini zaidi ya mwambao wa Kenya. Wanaume waliokuwa na silaha walimpiga risasi mwanamume wa Kingereza na kumteka nyara mkewe, ambaye anafikiriwa anazuwiliwa nchini …