Mwanajeshi wa Israeli kuachiliwa huru

MWANAJESHI mmoja wa Israeli Gilad Shalit, anatarajiwa kuachiliwa huru leo, baada ya kuzuiliwa kwa miaka mitano, huku wafungwa wa Palestina wapatao 1,000 wakiachiliwa huru kufuatia makubaliano na kundi la Hamas. Shalit mwenye umri wa miaka 25, alitekwa nyara mwaka wa 2006 na wanamgambo wa Hamas ambao walipitia njia za chini ya ardhini kuingia Israeli kutoka Gaza. Hapo jana mahakama ya …

Wafuasi wa Gaddafi waingia Mali

Wapiganaji wa kabila la Tuareg waliorudi Mali kutoka Libya wanaaminika kusaidia katika kuanzisha kundi jipya la waasi. Kundi hilo la National Movement for the Liberation la Azawad NMLA limesema ni matokeo ya muungano baina ya makundi mawili ya waasi, yaliyoongezwa nguvu na Watuareg waliopigana kwa ajili ya Kanali Muammar Gaddafi nchini Libya. Watuareg wa Mali wamelalamika kwa muda mrefu kwa …

Al-Shabbaab kukabiliana na majeshi ya Kenya- Somalia

Wanamgambo wa Al-Shabaab nchini Somalia wameahidi kulipiza kisasi dhidi ya wanajeshi wa Kenya walioingia katika ardhi ya Somalia kwa lengo la kuwatafuta raia wanne wa Ulaya waliotekwa nyara wiki iliyopita. Wanajeshi wa Kenya walivuuka mpaka na kuingia katika ardhi ya Somalia kiasi kilomita 100 kutoka eneo la mpaka wa kaskazini mwa Kenya hapo jana (16.10.2011), wakisaidiwa na helikopta. Hatua hiyo …

Vuguvugu la “occupy” linasambaa

Maandamano duniani kote ya kupinga kile waandamanaji wanakiona kama uroho na usimamizi mbaya wa uchumi duniani yameingia siku ya pili. Katika miji kadhaa – kutoka Auckland hadi Toronto – waandamanaji walikesha katika mahema kushinikiza wanasiasa wachukue hatua. Haijawa wazi iwapo maandamano yanaanza kushikamana na kuwa kitu kikubwa. Mjini London, msemaji alisema lengo ni kuiga mambo yanayotokea mjini New York, katika …

Upinzani Liberia kuyakataa matokeo ya uchaguzi

Vyama ninane vya upinzani, vikiwemo viwili ambavyo ni wapinzani wakuu wa Rais Ellen Johnson-Sirleaf vimesema kuwa vitayakataa matokeo ya uchaguzi wa urais uliyofanyika wiki hii vikidai kuwepo kwa wizi mkubwa wa kura. Kwa mujibu wa matokoe yaliyotolewa Ijumaa iliyopita, Rais Johnson-Sirleaf anaongoza kwa 45.4 ya kura dhidi ya mpizani wake mkuu Winston Tubman wa chama cha CDC aliyepata 29.5 asilimia …

Polisi wasaka madaktari waliotekwa Kenya

POLISI wakitumia helikopta na magari wanawasaka watu wenye silaha waliowateka nyara madaktari wawili wa Uhispania wanaofanya kazi na shirika la misaada la Medicins Sans Frontiers (MSF) karibu na mpaka na Somalia nchini Kenya. Wawili hao walitekwa katika kambi ya wakimbizi ya Daadab, ambayo inawahifadhi maelfu ya wakimbizi wanaokimbia njaa katika Pembe ya Afrika. Taarifa zinazohusianasomalia, kenya, ulaya Dereva wao, raia …