Trump Asema Atawafukuza Wasyria Akiwa Rais

Donald Trump amesema atafurusha wakimbizi kutoka Syria walio nchini Marekani iwapo atakuwa rais. Bilionea huyo, ambaye kwa sasa anaongoza kwenye kinyang’anyiro cha kusaka tiketi ya kuwania urais kupitia chama cha Republican amesema katika mkutano wa kisiasa New Hampshire: “Nikishinda, watarudi kwao.” Matamshi hayo ni tofauti na aliyoyatoa mapema mwezi huu akihojiwa na Fox News aliposema Marekani inafaa kuwapokea wakimbizi zaidi. …

Bendera ya Palestin Yapepea UN

Bendera ya Palestina imepeperushwa kwa mara ya kwanza katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York. Bendera hiyo ilipandishwa kwenye mlingoti kwenye sherehe iliyohudhuriwa na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas. Akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bw Abbas alisema ni jambo lisiloeleweka kwamba hadi sasa suala ya Palestina kuwa taifa bado halijatatuliwa. Alionya kuwa Mamlaka ya Palestina …

Jeshi Ladhibiti Kambi Burkina Faso

Serikali ya mpito ya Burkina Faso imesema jeshi limedhibiti kambi ya vikosi vya ulinzi vya Rais vilivyofanya mapinduzi mapema mwezi huu. Maafisa wametangaza tukio hilo kwa njia ya Televisheni, haijafahamika kama kuna madhara yeyote yalijitokeza. Awali, Mwandishi wa BBC mjini Ouagadougou alisema milio ya risasi na milipuko ilisikika na moshi kutapakaa kutoka eneo la kambi. Kiongozi wa mapinduzi,Jenerali Gilbert Diendere,ambaye …

Waafrika Wakutana Ujerumani Kuchangia na Kuombea Amani Senegali

Tokea mwaka 1982, serikali ya Senegali imekuwa ikipambana na Kundi la Movement of Democratic Forces of Casamance (MFDC), ambalo linapigania haki ya eneo la Casamance kujitenga, baada ya serikali kuu kushindwa kuzisimamia rasilimali za eneo hilo kwa usawa. Hizi ni harakati ambazo zimeshapoteza maisha ya Wasenegali wengi, na kwa bahati nzuri makubaliano ya kusitisha mapigano (Unilateral Ceasefire) yalifikiwa Mei 1, …

Mgomo Kenya; Walimu Waigomea Mahakama…!

UFUNDISHAJI masomo anuai katika shule za umma nchini Kenya umekwama licha ya amri ya mahakama ya kuwataka walimu ikilazimisha warejee shuleni Jumatatu. Mgomo wa walimu nchini Kenya umeingia wiki ya tano hivi sasa huku ufundishaji ukiendelea kuathirika. Vyama vya walimu nchini Kenya vimesema havitatekeleza amri ya mahakama iliyowataka kusitisha mgomo huo kwa siku tisini kuanzia leo. Badala yake vyama hivyo …

Kikosi cha Kumlinda Rais Chavunjwa Burkina Faso

Serikali ya Burkina Faso imevunja kikosa cha kumlinda rais ambacho kiliwashika mateka mawaziri wakati wa majaribio ya mapinduzi yaliyofeli. Hatua hiyo ilichukuliwa wakati wa mkutano wa kwanza wa serikali tangu siku ya Jumatano wakati rais wa mpito Michel Kafando aliporejeea madarakani. Image copyrightAFP Image caption Burkina Faso Waziri wa masuala ya ulinzi amefutwa kazi na tume imebuniwa kuwatambua wale waliohusika …