Kampuni mbili kubwa duniani za kuunda magari, zimeamua kushirikiana kiufundi, na kutengeneza magari ambayo hayatachafua sana mazingira. Toyota na BMW walitangaza ushirikiano huo wao mpya nchini Japan, siku chache kabla ya maonyesho ya magari kufunguliwa rasmi nchini humo. Kati ya mipango yao ya pamoja ni kutengeneza betri bora zaidi kutumika katika magari yanayotumia umeme. Makampuni mawili yanayoongoza kwa utengenezaji wa …
Mgambia atarajiwa kumrithi Ocampo ICC?
Fatou Bensouda anatarajiwa kutajwa kuwa mwendesha Mashtaka mkuu mpya wa Mahakama ya kimataifa ya ICC. Wakili huyo mwenye umri wa miaka 50 kutoka Gambia ni naibu wa Luis Moreno-Ocampo, ambaye muda wake unaisha mwakani. Awali alifanya kazi kama mwanasheria katika mahakama ya kimataifa ya Rwanda nchini Tanzania. Kesi zote za ICC mpaka sasa zinatoka Afrika, na baadhi ya viongozi wa …
Obama aitakia heri Tanzania maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru
Na Mwandishi Wetu RAIS wa Marekani, Barack Obama ametuma salamu za pongezi na kuitakia Tanzania maadhimisho mema ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Tanzania Bara inatimiza miaka 50 ya Uhuru, Desemba 9, 2011. Aidha, Rais Obama ameihakikishia Tanzania kuwa Marekani itaendelea kubakia rafiki na mshirika wa kuaminika katika jitihada za kuhakikisha kuwa Watanzania kujiletea maisha bora na kwa …
Wanawake wabakaji Zimbabwe wafikishwa Mahakamani
Polisi wa Zimbabwe wanaamini kuna mtindo wa wanawake kuwabaka wanaume Zimbabwe , ili kutumia mbegu zao za kiume katika ushirikina kujitajirisha. Imechukuwa zaidi ya mwaka mmoja polisi kuwakamata wahusika na siku ya Jumatatu wanawake watatu walifikishwa mbele ya mahakama katika mji mkuu Harare kwa mashtaka ambayo yameishangaza nchi nzima. Mtu mmoja aliyepitia madhila hayo hakutaka jina lake kutajwa, alielezea yaliomkuta …
Upigaji kura waongezwa muda DRC
Muda wa upigaji kura umeongezwa na kuingia siku ya pili katika baadhi ya maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo sehemu ambazo upigaji huo haukufanyika siku ya Jumatatu. Maafisa wa uchaguzi walisema kuongeza muda huo kunaathiri takriban watu 400 katika nchi hiyo kubwa yenye vituo vya kupigia kura 63,000. Mbali na hatua hiyo kuchukua muda mrefu, upigaji kura huo uligubikwa …
Wahusika wa kashfa ya BAE TZ kushtakiwa
Kundi la wabunge kutoka vyama mbali mbali vya siasa nchini Uingereza limetoa wito wa kufunguliwa mashtaka dhidi ya mtu yeyote aliyehusika katika kashfa ya ufisadi na rushwa kuhusiana na mauzo ya rada yaliyofanywa na kampuni ya vifaa vya ulinzi ya BAE Systems ya Uingereza. Kampuni ya BAE Systems tayari imekubali kulipa takriban dola millioni 46 kama fidia kwa Tanzania kwa …