Kabila atangazwa tena mshindi wa urais DRC

ALIYEKUWA Rais Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila ametangazwa tena kuwa ni mshindi wa urais wa taifa katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni. Kwa mujibu wa taarifa za Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo, Kabila ameshinda kwa asilimia 48, huku mpinzani wake mkuu, Etienee Thisekedi akiwa na asilimia 32.33 na Vital Khemere akiambulia asilimia 7.74. Awali ilitangazwa matokeo hayo yangelichelewa …

Mtoto wa Gaddafi ataka kukimbilia Mexico

*Mexico washtuka, wazuia mpango huo SERIKALI ya Mexico imesema imezuia njama iliyokuwa ifanywe na kundi la wahalifu la kumpenyeza kwa magendo mmoja wa watoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi nchini Mexico. Saadi Gaddafi amekuwa kwenye kifungo cha nyumbani nchini Niger iliyopo Afrika Magharibi tangu alipoikimbia Libya mwezi Septemba. Msemaji wa serikali ya Mexico, alisema Saadi Gaddafi na …

Kura rasmi za urais DRC kucheleweshwa

TUME ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema itachelewa kutangaza matokeo rasmi ya kura za urais kutokana na matatizo ya usafirishwaji wa nakala za kujumlishwa kwa kura. Taarifa zinasema matokeo ya awali yanaonesha rais wa sasa, Joseph Kabila (pichani juu) anaongoza akiwa mbele ya wapinzani wake ambao tayari umesema hautamtambua kiongozi huyo kama rais baada rais wa Congo. …

Laurent Gbagbo afikishwa mahakamani

RAIS aliyeondolewa madarakani nchini Ivory Coast, Laurent Gbagbo amefikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC). Laurent Gbagbo anakuwa ni rais wa kwanza kukabiliwa na mashtaka katika mahakama hiyo, huku akiwa ameshtakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu kwa kuhusishwa na umwagikaji damu uliotokea baada ya uchaguzi wenye utata mwaka jana. Gbagbo alipelekewa nchini Uholanzi wiki iliyopita. Kiongozi huyo …

Ivory Coast yakaribia kufanya uchaguzi

JUMUIA ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, inasema kuwa itatuma ujumbe wa wachunguzi 60 kusimamia uchaguzi wa bunge nchini Ivory Coast Desemba 11, 2011 kufuatia ombi la serikali ya nchi hiyo. Huo ni uchaguzi wa mwanzo kufanywa tangu uchaguzi wa rais wa mwaka 2010 uliokuwa na utata, na ambao ulizusha vita na kusababisha watu takribani 3,000 kuuwawa. Taarifa zaidi kutoka …

ICC yataka waziri wa ulinzi Sudan akamatwe

MWENDESHA Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Uhalifu wa Kivita (ICC), Luis Moreno-Ocampo ametuma maombi ya kukamatwa kwa Waziri wa Ulinzi wa Sudan, Abdelrahim Mohamed Hussein kwa tuhuma za uhalifu Darfur. Katika ufafanuzi wake Ocampo alisema Hussein anatuhumiwa kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhisi ya ubinadamu uliofanyika mwaka 2003-04, wakati huo, Hussein akiwa mwakilishi wa Sudan katika eneo lake la …