Wanajeshi wa Marekani waondoka Iraq

RAIS wa Marekani Barack Obama maeadhimisha kumalizika kwa vita vya Iraq kwa kupongeza “mafanikio yasiyo ya kawaida” kwa vikosi vya Marekani katika mapigano ambayo yalipingwa na wengi. Katika hotuba yake kwenye eneo la Fort Bragg mjini Carolina Kaskazini, aliwapongeza wanajeshi wale waliohudumu na hata kufariki dunia wakiwa vitani, pamoja na jamii zao. Wanajeshi wa Marekani wa mwisho kutoka nchini Iraq …

Marekani yasema uchaguzi DRC ulikuwa na dosari

MAREKANI imesema uchaguzi uliofanyika hivi karibuni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ulikuwa na dosari nyingi, hivyo kutaka mchakato wa tathmini urejewe upya. Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yamempa, Rais Joseph Kabila ushindi wa asilimia 49 dhidi ya asilimia 32 alizojipatia kiongozi wa upinzani na mpinzani mkuu wa Kabila, Etienne Tshisekedi. Taarifa kutoka Marekani zinasema, hata hivyo matokeo hayo yamekosolewa …

ICC yaifikisha Malawi Umoja wa Mataifa

MAHAKAMA ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imeifikisha nchi ya Malawi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kukataa kumkamata Rais wa Sudan Omar al-Bashir. Malawi ilikuwa mwenyeji wa Rais Bashir mwezi Oktoba licha ya kufahamu kuwa kuna kibali cha ICC cha kumkamata kwa tuhuma za mauaji ya kimbari katika eneo la Darfur mtuhumiwa huyo. Taarifa kutoka ICC zinasema …

Rais Kabila akanusha kuiba kura DRC

RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila amekanusha vikali madai ya kwamba alishinda uchaguzi wa nchi hiyo kupitia wizi wa kura. Waangalizi kutoka wakfu wa Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter walisema matokeo ya uchaguzi huo hayakuwa ya kuaminika, na pia Askofu wa mkuu wa kanisa Katoliki mjini Kinshasa akasema matokeo hayo hayakudhihirisha ukweli halisi. Taarifa zaidi …

Uchaguzi DRC utata mtupu, waangalizi watofautiana

UJUMBE wa Kimataifa wa wasimamizi wa uchaguzi umetamka kuwa ni kweli uchaguzi uliofanywa katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, ulikuwa na dosari kadhaa hivyo si wa kutegemewa. Hata hivyo, tayari Rais Kabila alishinda katika uchaguzi huo. Kituo cha Carter kimesema kuwa uchaguzi huo umetiwa dosari, kwa kutotayarishwa sawasawa, na pengine ulikuwa na udanganyifu. Taarifa zaidi zinaeleza kuwa matokeo ya vituo …

Urusi kwachafuka, maelfu waandamana

MAELFU ya wananchi nchini Urusi wameandamana katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo wakishinikiza kurudiwa kwa Uchaguzi wa Bunge uliofanywa Jumapili iliyopita nchini humo. Taarifa kutoka ndani ya Mji Mkuu wa nchi hiyo, Moscow, zinasema maandamano makubwa yamefanywa katika Mji huo, ambako mwandishi wa BBC, anasema maelfu ya watu wako katika medani, ng’ambo ya pili ya mto, mkabala na Ofisi za …