Watu takriban 15 wauwawa kwenye mlipuko Myanmar

WATU takriban 15 wameuwawa na wengine 79 kujeruhiwa kufuatia mlipuko uliotokea katika mji mkuu wa Myanmar, Yangon. Maafisa wanasema mlipuko huo ulisababisha moto kwenye ghala linalomilikiwa na serikali, ambao ulienea kwa kasi katika makazi ya watu na majengo mengine yaliyokuwa karibu, mengi yao yakiwa ya mbao. Wazima moto wanaendelea na juhudi za kuuzima moto huo na kuzitafuta maiti. Duru za …

Kesi ya Mubarak kuendelea Misri

KESI ya aliyekuwa rais wa zamani wa Misri ,Hosni Mubarak inaanza imeanza tena tarehe 28.12.2011 mjini Cairo, baada ya kipindi cha miezi mitatu kilichoshuhudia machafuko ya umwagaji damu na vyama vya Kiislamu vikishinda uchaguzi wa bunge. Mubarak mwenye umri wa miaka 83 anashtakiwa kwa kuamuru mauaji ya watu takriban 850 wakati wa maandamano ya mapinduzi ambayo hatimaye yalimuondoa madarakani. Anakabiliwa …

Korea Kaskazini yamzika Kim Jong -il

Korea Kaskazini inafanya maziko ya kitaifa ya kiongozi wake Kim Jong-il huku msafara mkubwa wa magari yaliyosindikiza jeneza la kiongozi huyo ukipitia mji mkuu Pyongyang. Picha cha runinga zimeonyesha maelfu ya wanajeshi wakitoa heshima za mwisho kwa picha ya kiongozi huyo iliyopitia kwenye barabara za mji. Mridhi wa uwongozi ambaye ni mwanawe wa kiume Kim Jong-Un amezindikisha jeneza la babake …

Washukiwa ugaidi waachiliwa Kenya

WATU hao ambao ni raia wa Kenya na picha zao zilisambazwa kwa umma kabla, walijisalimisha wenyewe kwa wakuu Jumamosi iliopita. Vita dhidi ya ugaidi nchini Kenya vimekosolewa, huku polisi wakishutumiwa kutokuwa makini katika uchunguzi wao . Msemaji wa polisi nchini Kenya, Eric Kiraithe aliiambia BBC, kwamba bado wako imara katika kupambana na ugaidi licha ya washukiwa hao kuachiliwa huru. Na …

Msimamo mkali wa dini wapingwa Israil

Rais Shimon Peres wa Israil alisema wachache nchini Israil wanafanya vitendo vya aibu na wanavunja umoja wa taifa. Aliwahimiza watu wajiunge na maandamano hayo katika mji wa Beit Shemesh, karibu na Jerusalem. Mji huo umezusha hasira nchini Israil, tangu msichana wa miaka minane aliposema anaogopa kwenda shule, baada ya wanaume wa Kiyahudi wenye msimamo mkali kumtemea mate, na kumshutumu kuwa …

Mfululizo wa milipuko ya mabomu waitikisa Nigeria

MILIPUKO ya mabomu imeendelea mfululizo katika maeneo kadhaa nchini Nigeria wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Krismasi, ambapo hadi sasa yameshasababisha vifo vya watu 28 na wengine kadhaa kuachwa majeruhi. Mlipuko wa kwanza ulitokea asubuhi ya leo katika Kanisa la Mtakatifu Theresa kwenye mtaa wa Madalla, mjini Abuja, wakati waumini wakishiriki sala ya Krismasi. Miripuko mingine imetokea mchana katika miji …