Maisha 2012 hayashikiki-Watabiri

IMETABIRIWA kuwa mwaka 2012 utakuwa mwaka mwengine mbaya kiuchumi kwa bara la Ulaya, ingawa ahuweni ya kiuchumi katika masoko yanayoinukia na Marekani huenda ikaufanya uchumi wa dunia kutokupoteza muelekeo moja kwa moja. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na shirika la habari la Reuters, hakuna sababu za kuufurahikia mwaka wa 2012. Mataifa mengi makubwa duniani yanaelekea kwenye mtikisiko wa kiuchumi, masoko …

Mwanamuziki Senegal atangaza kugombea urais

MWANAMUZIKI mashuhuri nchini Senegal na mwanaharakati wa kisiasa,Youssou N’dour, ametangaza kuwania kiti cha urais katika uchaguzi wa mwezi Februari nchini humo. Mwanamuziki huyo amesema kuwa anaitikia wito wa kumtaka agombee kiti hicho dhidi ya rais wa sasa Abdoulaye Wade, ambaye anapania kuwania kiti hicho kwa muhula wa tatu. Youssou N’dour amehusika na maswala ya kibinadamu kwa siku nyingi na pia …

Al- Mahmoundi kurudishwa Libya

RAIS wa Tunisia, Moncef Marzouki, amesema nchi hiyo haitamuwasilisha kwa mashtaka nchini Libya aliyekuwa waziri mkuu wa Libya, Baghdadi Al-Mahmoudi, bila ya hakikisho kwamba atashtakiwa kwa njia iliyo huru na haki na kwamba atalindwa. Libya inamsaka Bwana Al-Mahmoudi kwa tuhuma za kutumia vibaya mamlaka. Al-Mahmudi alitorokea nchini Tunisia punde baada ya Kanali Gaddafi kupinduliwa na anameshikiliwa nchini humo. Akiwa ziarani …

Mji wa Sudan Kusini watekwa

MJI wa Pibor ulitekwa na kabila la Lou Nuer Jumamosi, ingawa kulikuwa na askari wa Umoja wa Mataifa hapo pamoja na wanajeshi wa serikali. Shirika la msaada wa matibabu la kimataifa, MSF, linasema kuwa lina wasiwasi mkubwa juu ya wafanyakazi wao zaidi ya 150 ambao wamekimbilia vichakani, wakati wa shambulio hilo, lilofanywa na maelfu ya watu wa kabila la Lou …

Iran yajaribu kombora jipya

IRAN inasema imefanya jaribio la kurusha kombora la masafa ya wastani. Jaribio hilo lilifanywa wakati wa mazoezi ya jeshi karibu na Hormuz, mlango unaounganisha Ghuba na Bahari ya Hindi. Jeshi la wanamaji la Iran linasema siku ya mwisho ya mazoezi Jumatatu, meli zitaweza kupita kwenye njia ya Hormuz, ikiwa tu jeshi hilo litaziruhusu. Mkondo wa Hormuz ni njia inayopitwa na …

Shambulio la Garissa Al-shabaab wausishwa watano wauwawa

WATU WATANO wameuwawa na zaidi ya 20 kujeruhiwa kwenye klabu ya starehe mjini Garissa, kaskazini-mashariki mwa Kenya. Washambuliaji walirusha maguruneti kwenye klabu hiyo na kisha kuwapiga risasi watu waliojaribu kukimbia. Mji wa Garissa uko karibu na mpaka wa Somalia ambako jeshi la Kenya lilingia mwezi wa Oktoba, kuwaandama wapiganaji wa al-Shabaab. Polisi wanasema watu waliohusika na al-Shabaab huenda walifanya shambulio …