Waliokufa ajali ya meli Italia wafikia watano, 17 hawaonekani

MAITI mbili zimeopolewa tena katika meli kubwa ya kifahari ya abiria ya Costa Concordia iliyozama juzi nchini Italia eneo la Kisiwa cha Giglio. Kupatikana kwa maiti hizo kunafanya idadi ya abiria waliokuwa katika meli hiyo kufikia tano. Mlinzi wa jirani na ajali hiyo alisema maiti za wanaume wawili wazee zimeopolewa katika upande uliozama wa meli, huku taarifa zingine zikidai bado …

Mgomo Nigeria washingwa kupatiwa suluisho, mazungumzo yavunjika

MAZUNGUMZO baina ya Serikali ya Nigeria na Vyama vya Wafanyakazi kuhusu fidia ya bei ya mafuta yamevunjika, na sasa kuna uwezekano mkubwa kwa wafanyakazi wa visima vya mafuta nao watajiunga na mgomo ulioendelea kwa juma zima. Taarifa zinasema katika mkutano wa jana usiku Vyama vya Wafanyakazi viliitaka Serikali irejeshe kwa ukamilifu fidia ya bei ya mafuta, ama sivyo wataendelea kugoma …

Meli yapinduka Italia, yaua 3, abiria 50 wapotea

VIKOSI vya uokoaji majini nchini Italia vimeanza kuikagua Meli ya Costa Concordia iliyopinduka upande mmoja baada ya kwenda mrama nje ya pwani ya magharibi Ijumaa usiku na kuuwa watu watatu. Abiria wanasema walisikia kishindo kikubwa kabla ya meli hiyo, Costa Concordia, kutikisika na kusimama na taa kuzimika. Mlinzi mmoja wa pwani alisema inasadikika meli hiyo iligonga kitu ambacho kiliipasua meli …

Marekani yakerwa maiti ‘kukojolewa’ na askari

WAZIRI wa Ulinzi wa Marekani, Leon Panetta amesema video inayoonesha askari wa Jeshi la Majini la Marekani wakikojolea maiti za Wafghanistan ni la “kusikitisha sana”. Alisema, wale walioshiriki katika tukio hilo kwa namna moja au nyingine watachukuliwa hatua “kali sana”. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Asia zinasema video hiyo, iliyowekwa kwenye mtandao, imekusudia kuonesha wanajeshi wanne wa majini wakiwa wamesimama …

Maseneta wa US wakataa mashoga jeshini

MASENETA wa chama cha Republican nchini Marekani wamepinga pendekezo la kuwaruhusu wapenzi wa jinsia moja kuhudumu wazi katika jeshi la Marekani. Wamedai kuwa uwezo wa jeshi utavurugwa na kurudisha nyuma sera zilizopo zinazofahamika kama ‘Usiulize,Usiseme.’ Maseneta wawili wa chama cha Democrat waliungana na wale wa Republican kutupilia mbali mageuzi ambayo yaliungwa mkono na rais Obama. Rais Obama alipigia debe mabadiliko …

Kashfa ya ngono yamtafuna mgombea urais-Marekani

MWANASIASA mashuhuri anayegombea tiketi ya urais ya chama cha Republicans nchini Marekani, amekanusha madai mapya kuwa alijaribu kumlazimisha mwanamke mmoja kufanya mapenzi naye. Herman Cain anaongoza wanaogombea tiketi hiyo ilikukabiliana na Rais Barack Obama kwenye uchaguzi mwakani. Akizungumza kwenye runinga ya ABC, Bw Cain amesema madai hayo ni ya uongo na atayajibu ipasavyo katika mkutano na waandishi wa habari leo …