MAHAKAMA ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) ya The Hague, Uholanzi, imewatia hatiani watuhumiwa wanne kati ya sita wa Kenya wanaotuhumiwa na ghasia zilizoikumba nchi hiyo baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007. Taarifa ambazo mtandao huu umezipata mchana huu watuhumiwa hao sasa watakuwa na kesi ya kujibu kuhusiana tuhuma zinazowakabili. Hata hivyo bado majaji hawajaweka hadharani majina yao. …
Hatma ya washukiwa vurugu za uchaguzi Kenya leo
*ICC kutamka wana makosa au la! MAHAKAMA ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) iliyoko mjini The Hague, Uholanzi, leo itasema kama Naibu Waziri Mkuu wa Kenya, Uhuru Kenyatta pamoja na wenzake watano mashuhuri wana kesi ya kujibu kuhusiana na tuhuma za kuhusika katika ghasia zilizoikumba nchi hiyo baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007. Inasadikiwa kuwa katika vurugu hizo …
Mashambulio ya wanawake wavaa suruali yakithiri Malawi
TAKRIBANI watu 3,000 wamekusanyika Blantyre nchini Malawi kupinga mashambulio dhidi ya wanawake wanaovaa suruali. Baadhi ya wachuuzi wa kike wiki hii walipigwa na kuvuliwa nguo kwenye mitaa ya mji mkuu, Lilongwe, na Blantyre kwa kutovaa mavazi ya asili. Mmoja aliyeandaa maandamano hayo amesema amewasihi wanawake kujitokeza wakiwa wamevaa suruali na fulana nyeupe kuonyesha kukasirishwa kwao. Rais Bingu wa Mutharika alisema …
Milipuko yatikisa mji wa Kano, Nigeria al-shabab yahusishwa
Watu kadhaa wameripotiwa kuuawa kwenye milipuko iliyotokea katika mji wa Kano, kaskazini mwa Nigeria. Vituo vya Polisi pamoja na makao makuu ya Polisi eneo hilo ni miongoni mwa sehemu zilizolengwa katika mashambulizi hayo. Milio ya risasi pia imesikika katika sehemu kadhaa. Kundi la kiislamu la Boko Haram limesema ndilo lililotekeleza mashambulizi hayo. Kundi hilo ndilo limekuwa likiendesha ghasia katika siku …
Kiongozi wa Boko Haram aliyekuwa chini ya ulinzi atoweka
*Ni baada ya msafara wa Polisi Nigeria kushambuliwa IDARA ya Polisi nchini Nigeria, imethibitisha kuwa mshukiwa mmoja ambaye anaaminika kuwa kiongozi wa Kundi la Boko Haram, ametoweka, baada ya wapiganaji wa kundi hilo kushambulia msafara wa polisi ambao ulikuwa ukimpeleka kizuizini. Mshukiwa huyo alikuwa amekamatwa na polisi siku ya Jumamosi na alikuwa akisafirishwa korokoroni ili kuwapa maofisa wa polisi nafasi …
Mauaji yashamiri Sudan Kusini
WATU wenye silaha wamewaua takriban watu 51 wengi wakiwa wanawake na watoto katika mapigano ya hivi karibuni katika jimbo lenye mgogoro la Jonglei, gavana wa jimbo hilo Kuol Manyang amesema. Taarifa zinasema kuwa kiasi cha watu 22 wamejeruhiwa baada ya washambuliaji kuvamia na kuchoma kijiji cha Duk Padiet, aliongeza. Waliojeruhiwa wamehamishiwa Juba makao makuu ya nchi. Mfululizo wa mashambulizi ya …