Matokeo ya ubunge DRC yatangazwa

*Kabila ashinda viti vingi bungeni MATOKEO ya uchaguzi ya ubunge katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yametangazwa karibu katika maeneo mengi na Chama tawala cha PPRD kimenyakuwa idadi kubwa ya viti 58, huku muungano wa vyama vinavyoiunga Serikali ikiwa imepata idadi kubwa ya viti vilivyonyakuliwa na muungano wa upinzani unaomuunga mkono, Etienne Tshisekedi. Imeichukua tume huru ya uchaguzi katika Jamhuri …

Kenyatta aachia ngazi

WAZIRI wa Fedha wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameachia nafasi yake kufuatia uamuzi kuwa atashtakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu. Hatua hiyo inakuja baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kusema kiongozi huyo anakabiliwa na mashtaka kuhusiana na ghasia kubwa za Kenya zilizozuka baada ya uchaguzi nchini humo mwaka 2007. Hata hivyo anabaki kuwa Naibu Waziri Mkuu, kwa …

Naibu Jaji Mkuu Kenya asimamishwa kazi

*Yaundwa tume chini ya Jaji Mtanzania kumchunguza RAIS wa Kenya, Mwai Kibaki amemsimamisha kazi Naibu Jaji Mkuu, Nancy Baraza na kuunda jopo la majaji ambalo litachunguza mwenendo wa kazi wa kiongozi huyo kutokana na tuhuma zinazomkabili. Taarifa zimesema Jaji Baraza, anatuhumiwa kumtishia maisha kwa bastola mlinzi wa duka moja kubwa, Bi Rebecca Kerubo wakati wa mkesha wa mwaka mpya. Jopo …

Ocampo kuendelea kuwabana Kosgey na Ali

*Asema anatafuta ushaidi mwingine KIONGOZI Mkuu wa Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), ya mjini The Hague, Louis Moreno Ocampo amesema atawasilisha ushahidi zaidi kutaka mashtaka yathibitishwe dhidi ya Wakenya wawili mashuhuri, ambao majaji katika mahakama hiyo walikataa kuthibitisha mashtaka dhidi yao kuhusiana na ghasia za baada ya uchagzui wa mwaka 2007 nchini Kenya. Jumatatu hii Mahakama ya …

Kibaki awataka Wakenya kuwa watulivu

RAIS wa Kenya, Mwai Kibaki amewataka raia wote wa nchi hiyo kuwa watulivu hasa baada ya uamuzi wa Mahakama ya Jinai Kimataifa (ICC) kuwatia hatiani wakenya wanne kati ya sita waliyokuwa wakikabiliwa na uhalifu wa kibinadamu. “Nchi hii yetu tukufu imekuwa na changamoto kubwa,” Mwai Kibaki alisema katika taarifa yake. Kenyatta mtoto wa rais wa kwanza wa Kenya na mtu …