CHINA na Urusi zimendelea kushutumiwa vikali kwa kutumia kura ya turufu kupinga azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kumaliza ghasia nchini Syria, ambako mauaji dhidi ya waandamanaji yanaripotiwa kuendelea. Mwanaharakati wa vuguvugu la mageuzi katika ulimwengu wa Kiarabu ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Nobel, Tawakkul Karman, ameulaani vikali utawala wa Bashar al-Assad. Mtetezi huyo …
37 wauawa Sudan Kusini
WATU wapatao 37 wameuawa nchini Sudan Kusini baada ya kushambuliwa kwa risasi kwenye mkutano wa amani unaolenga kumaliza ghasia katika eneo hilo, wamesema maofisa nchini humo. Maofisa kutoka majimbo matatu walikutana katika mazungumzo yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa katika mji wa Mayendit, kwenye jimbo la Unity, katika jitihada za kupunguza uhasama wa kikabila. Taarifa zaidi kutoka Sudan Kusini, zinasema kuwa …
Baa la njaa limekwisha Somalia
UMOJA wa Mataifa (UN) umetangaza kuwa baa la njaa nchini Somalia lililotangazwa kulikumba taifa hilo hivi karibuni sasa limefikia kikomo. Umoja huo umesema hali imeimarika nchini humo kutokana na mavuno mazuri na misaada ya kibinadamu inayoendelea kutolewa. Taarifa ndani ya Somalia zinasema; mwezi uliopita mshiriki mkuu wa shughuli za umoja huo nchini Somalia, Mark Bowden alisema maelfu ya watu wamekufa …
Kenya yatakiwa kumkamata Henry Banda
NCHI ya Kenya imepokea ombi kutoka kwa Shirika la Polisi wa Kimataifa Interpol kumkamata mwana wa kiume wa rais wa zamani wa Zambia Rupiah Banda anayeaminika kutorokea nchini humo. Henry anasemekana kuondoka nchini Afrika Kusini na sasa yuko mafichoni nchini Kenya. Anatafutwa kuhusiana na sakata ya mauzo ya mali ya kampuni ya mawasiliano ya simu ya Zamtel, inayomilikiwa na Serikali. …
Rais Wade wa Senegal kugombea urais tena
MAHAKAMA Kuu ya Senegal imetupilia mbali kesi ya rufaa ya vyama vya upinzani na kuamua kuwa Rais Abdoulaye Wade anaweza kugombea tena kiti cha urais wa nchi hiyo kwa mara ya tatu. Upinzani umesema Katiba ya nchi hiyo imeweka kikomo cha mihula miwili, lakini mahakama hiyo imesema, Wade hafungwi na sheria hiyo kwa sababu, sheria hiyo ilipitishwa akiwa katika muhula …
Boko Haram wauwawa Nigeria
JESHI la Nigeria linasema limewapiga risasi na kuwauwa wafuasi 11 wa kikundi cha wapiganaji wa Kiislamu, Boko Haram, kaskazini-mashariki mwa nchi. Msemaji wa jeshi alieleza kwamba wapiganaji hao waliuwawa wakati wa mapambano katika mji wa Maiduguri, ambako kundi hilo lilianzishwa mwongo uliopita. Juma lilopita watu kama 185 waliuwawa katika mji mwengine wa kaskazini, Kano, kwenye mashambulio kadha ya mabomu. Boko …