Viongozi Somalia wakubaliana

VIONGOZI wa Somalia wametia saini mkataba ambao wanataraji utamaliza mvutano na mgogoro uliopo katika nchi hiyo. Katika makubaliano hayo wameridhia kuwepo kwa Bunge jipya pamoja na baraza la pili la wazee na Serikali za Majimbo. Makubaliano hayo yaliyotiwa saini na Serikali ya sasa, utawala wa majimbo mawili, na wanamgambo wanaounga mkono Serikali, yatajadiliwa juma lijalo, kwenye mkutano wa London kuhusu …

UN yapitisha azimio kulaani vitendo vya Syria

BARAZA Kuu la Umoja wa Mataifa(UN) limeidhinisha kura ya azimio kuhusu Syria sawa na ile iliyopigiwa kura ya turufu na Urusi na Uchina katika baraza la usalama la umoja huo. Zaidi ya theluthi mbili ya wanachama wa baraza kuu la umoja wa mataifa waliunga mkona azimio hilo. Taarifa zaidi zinasema azimio hilo linalaani mashambulizi yanayofanywa na Serikali ya Syria dhidi …

Mawaziri wawili wajiuzulu nchini Uganda

MAWAZIRI wawili ambao waliamuliwa kuwajibika nakuisababbishia serikali hasara ya dola milioni 60, kutokana na malipo ya kufidia mfanya biashara baada ya kupoteza umilikaji wa soko kadhaa mjini Kampala, wamejiuzulu. Hii inatokana na mapendekezo ya tume iliyochunguza matumizi ya mali ya Umma. Taarifa kutoka Uganda zinasema, aliekuwa waziri aliehusika na masuala ya jinsia pamoja na waziri mwingine katika ofisi ya waziri …

Watu 28 wauwawa kwa mabomu Urusi

MABOMU mawili yaliyotegwa katika magari yakilenga vituo vya usalama katika Mji wa Aleppo yameuwa takribani watu 28, huku waasi wakiishutumu Serikali ya nchi hiyo wakianzisha mashambulizi ili kuepuka lawama. Milipuko hiyo iliyotokea jana Ijumaa ilitokea wakati vifaru pamoja na vikosi vya jeshi vikisonga mbele kupambana na vikundi vya waasi katika mji ambao ni ngome kuu ya upinzani wa Homs, na …

Al-Shabaab yaungana rasmi na Al-Qaeda

KUNDI la Waislamu wenye itikadi kali nchini Somalia, Al-Shabaab, limetangaza kuungana na kundi la Al-Qaeda. Tamko hilo limetolewa katika picha ya video iliyotolewa na makundi hayo mawili. Taarifa zaidi kutoka nchini Somalia zinasema, Yusuf Garaad wa Idhaa ya Kisomali ya BBC ambaye ameitazama video hiyo amesema kundi hilo ambalo jina lake kamili ni Harakat al Mujahiddin al Shabaab, limetangaza rasmi …

Fatah na Hamas wafikia mwafaka

BAADA ya miaka mingi ya mivutano na uhasama baina ya kundi la Hamas na chama cha Fatah ndani ya Palestina, hatimae makundi hayo yamefikia maridhiano ya kuwa na serikali ya mpito ya Umoja wa Kitaifa. Makubaliano hayo yamefikiwa leo huko Doha, nchini Qatar, kati ya kiongozi wa chama cha Fatah, Rais Mahmoud Abbas, na kiongozi wa Hamas, anayeishi uhamishoni, Khaled …