ZAO la muhogo linaweza kusaidia wakulima wa Afrika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, taarifa za wanasayansi zinasema. “Ni zao linalostahamili ukame kuliko mazao yote ya chakula,” amesema Kiongozi wa ripoti, Andy Jarvis, wa Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa Mazao ya Kilimo ya nchi za joto, Colombia. “Wakati mazao mengine makuu yanaweza kuangamizwa na joto na matatizo mengine …
Rais mpya Yemen anusurika kulipuliwa kwa bomu
RAIS mpya wa Yemeni, Abd-Rabbu Mansour amenusurika kulipuliwa na bomu baada ya bomu kubwa lilotegwa kwenye gari, nje ya nyumba yake, Kusini mwa Yemen, mjini Mukalla, kulipuka na kuuwa watu wapatao 20. Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema shambulio limefanywa wakati rais mpya Abd-Rabbu Mansour Hadi akiapishwa. Rais huyo amechukua kiti cha Ali Abdullah Saleh, ambaye ameongoza nchi kwa miaka …
Wapiganaji 6 wa al-Shabaab wauawa
WAPIGANAJI sita wa kigeni kutoka kundi la Kiislamu la Al-Shabaab wameuawa kwenye shambulio la anga lililotekelezwa Kusini mwa Somalia. Walioshuhudia tukio hilo wanasema, watu 6 waliuawa wakiwemo raia kadhaa wa kigeni. Magari mawili yaliharibiwa wakati wa shambulio hilo la anga lililofanyika katika eneo linalojulikana kama K60 takriban 60km kutoka mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu. Taarifa zilizoripotiwa na BBC mjini …
Uingereza yasema Somalia lazima isaidiwe
MKUTANO wa kimataifa kuhusu hatma ya Somalia umemalizika mjini London kwa Serikali ya Uingereza pamoja na Marekani zikisisitiza nchi hiyo lazima isaidiwe kusimama tena na kuwa nchi thabiti na yenye amani. Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, akifunga mkutano huo amesema yalioafikiwa katika mkutano huo ni jinsi ya kumaliza uharamia, kutoa misaada ya kibinadamu, usalama na kulitokomeza kundi la Al …
Wanajeshi 5,700 zaidi kupelekwa Somalia
BARAZA la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) linatarajiwa kupiga kura ya kuidhinisha jeshi la kulinda usalama nchini Somalia kuongezwa kwa zaidi ya wanajeshi 5,000. Taarifa zaidi zinasema, hali hiyo itafanya idadi ya wanajeshi wote wa kuhifadhi amani walio Somalia kufikia 17,731. Hadi sasa kuna jumla ya wanajeshi 12,000 wa kigeni nchini humo. Kura hiyo ya Baraza la Usalama kutaipa …
Wanaume nchini Kenya kugoma kula majumbani
WANAUME nchini Kenya wanapanga kugomea vyakula vya mabibi zao kwa siku sita kutoka na kuongezeka kwa visa vya wanawake kuwapiga mabwana zao na badala yake wanaume hao watakuwa wakila hotelini na magengeni (kwa akina mama na baba lishe) Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo ya Kina Baba nchini humo, Nderitu Njoka amesema mgomo huo wa …