Milipuko yauwa wasafiri Nairobi

WATU watano wameuwawa na wengi zaidi ya 40 kujeruhiwa kwenye shambulio katika Kituo cha Basi cha Machakos mjini Nairobi, Kenya. Taarifa zinasema kuwa maguruneti kama mane yalirushwa kutoka kwenye gari dhidi ya kituo cha basi cha Machakos Bus Station mjini Nairobi, ambacho kilikuwa kimejaa watu muda huo. Shambulio hilo limetokea Jumamosi majira ya saa moja na nusu usiku. Hadi sasa …

Maelfu kukumbwa na njaa eneo la Sahel

SHIRIKA la misaada la Uingereza Oxfam, limeonya kuwa huenda kukatokea janga kubwa la kibinadam katika eneo la Sahel Afrika Magharibi kutokana na ukame mkubwa unaoendelea katika eneo hilo iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa. Shirika hilo limeanzisha kampeini ya kuomba msaada wa dola milioni thelathini na sita kuwasaidia watu katika eneo hilo. Athari za ukame huu na bei ya juu ya …

Wauguzi elfu 25 waliogoma wafutwa kazi Kenya

SERIKALI nchini Kenya imewafukuza kazi wauguzi 25,000 waliogoma kwa kushindwa kurudi kazini. Msemaji wa Serikali hiyo, Alfred Mutua amewataka watu wote wenye taaluma ya afya na ambao hawakuwa na ajira au waliostaafu kufika hosiptali za umma kwa ajili ya kuajiriwa siku ya Ijumaa kuziba nafasi ya wauguzi hao. Taarifa kutoka Kenya zinasema wafanyakazi wa umma ambo wengi ni manesi waligoma …

Meli ya ng’ombe yazuiwa kuegesha Misri

WATETEZI haki za wanyama wameiomba Misri na Djibouti zikubali meli yenye matatizo na iliyosheheni maelfu ya ng’ombe itie nanga katika bandarini moja wapo. Shirika liitwalo “Huruma kwa Wanyama” linasema kuwa limepata taarifa kuwa ng’ombe karibu 3,000, waliopo kwenye meli hiyo ya Gracia del Mar, wameshakufa. Meli hiyo imetia nanga kwenye Bahari ya Sham, tangu ilipopata matatizo kwenye mitambo na imekataliwa …

Mradi Mkubwa Bandari Lamu wazinduliwa

MRADI mkubwa umezinduliwa Pwani ya Lamu ambao utaziunganisha nchi za Kenya, Ethiopia na Sudani Kusini. Ujenzi wa mradi huo mkubwa wa bandari unatarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 23 (£14.5bn), na utakuwa Kusini Mashariki mwa pwani ya nchi ya Kenya kwenye Mji wa Lamu mpakani mwa Somalia. Mradi huo utajumuisha pia ujenzi wa bomba la mafuta, reli na barabara kuunganisha …

Chama cha ANC Afrika Kusini chamtimua Malema

CHAMA tawala cha ANC nchini Afrika Kusini kimemtimua rasmi kiongozi wa Jumuiya ya vijana katika chama hicho, Julius Malema, baada ya rufaa ya kupinga uamuzi wa kutimuliwa kwake hapo awali kutupiliwa mbali. Kamati ya Nidhamu ya ANC ilitoa uamuzi huo baada ya kusikiliza rufaa iliyowasilishwa na Malema dhidi ya kutimuliwa kwake uanachama kwa kipindi cha miaka mitano kwa makosa ya …