Wakimbizi wauliwa na kombora Somalia

WAKIMBIZI sita wa Kisomali wameuwawa katika shambulio la kombora mjini Mogadishu Somalia. Vifo vilitokea baada ya makombora kuangukia kambi moja ya wakimbizi karibu na ikulu ya rais mjini Mogadishu. Taarifa zaidi kuhusiana na shambulio hilo zinaeleza kuwa mbali na vifo hivyo pia inasadikiwa watu watano walijeruhiwa kwenye shambulio hilo. Haijulikani aliyefanya shambulio hilo lakini wiki jana kundi la wapinaji wa …

Ujerumani yapata rais mpya

MWANAHARAKATI wa zamani wa haki za binaadamu nchini Ujerumani Joachim Gauck amechaguliwa kuwa rais mpya wa Ujerumani siku ya Jumapili, Machi 18, 2012. Gauck amekuwa mgombea wa kwanza kutoka iliokuwa Ujerumani Mashariki kuongoza nchi, akiwekewa matumaini makubwa kwamba atarudisha heshima katika ofisi hiyo ya rais kufuatia kashfa zilizowasibu watangulizi wake wawili. Gauck mwenye umri wa miaka 72 alijizolea kura 991 …

Alietengeneza filamu ya Joseph Kony arukwa na akili

MKURUGENZI wa filamu, Jason Russell, ambaye filamu yake inayomshambulia kiongozi wa wapiganaji wa Uganda, Joseph Kony, ilizagaa kwenye mtandao wa internet, inanaiwa amepata ugonjwa wa akili. Shirika lililofanya filamu hiyo, liitwalo “Invisible Children”, limesema kuwa Russell amelazwa hospitali kutokana na machofu, kiwiliwili kuwa kikavu, na njaa. Shirika la “Invisible Children”, lilisema zogo lilozuka baada ya filamu hiyo, limesumbua roho za …

Mwanajeshi wa Marekani aliyeua raia 16 alifadhaika

INADAIWA kuwa mwanajeshi wa Marekani anayetuhumiwa kuwauwa raia 16 Kusini mwa Afghanistan alifanya hivyo baada ya kufadhaishwa kwa kitendo cha kupelekwa vitani kwa mara ya nne bila yeye kutarajia, lakini familia yake imestushwa na tukio alilolifanya. Wakili wa mshukiwa huyo, John Henry Browne ameliambia shirika la habari la AP kuwa mteja wake alikuwa amehakikishiwa kuwa hangepelekwa tena katika eneo la …

Nembo za HIV shuleni Tanzania zakera

WANAHARAKATI nchini Tanzania wameelezea kughadhabishwa na hatua ya baadhi ya shule nchini humo kuwataka wanafunzi wanoishi na virusi vya HIV kuvaa riboni nyekundu kwenye sare zao za shule wakiwa shuleni. Mwalimu Mkuu wa shule moja ameambia BBC kuwa kitendo hicho kilifanyika kufuatia ombi la wazazi kuhakikisha kuwa wanafunzi wagonjwa hawapewi majukumu ambayo huenda yakaathiri afya yao. Lakini ubaguzi kama huu …

Mamia wauawa Sudan Kusini kwa kisasi

WATU takriban 100 wameuawa Sudan Kusini katika mfululizo wa mauaji ya kikabila hivi karibuni na wizi wa mifugo, maafisa wamesema. Waziri wa sheria wa Jimbo la Jonglei, Gabriel Duop Lam aliambia BBC kuwa takriban watu 200 wengine wamejeruhiwa. Mwandishi wa BBC James Copnall, mjini Khartoum, anasema takwimu hizo zinaashiria kuwa kuna idadi kubwa zaidi. Wizi wa ng’ombe na mashambulizi ya …