MALI inaweza kuwekewa vikwazo hii leo, baada ya viongozi wa kijeshi kutoonesha ishara zozote kuheshimu ahadi walizotoa za kurejesha utawala wa kiraia nchini humo. Muda wa saa 72 uliowekwa na Jumuia ya uchumi ya nchi za Afrika magharibi-ECOWAS, ili wanajeshi warejee kambini umemalizika saa sita usiku, jana kuamkia leo. Viongozi wa mataifa ya Afrika Magharibi wanakutana Dakar leo kuzungumzia hali …
Viongozi wa ECOWAS wasitisha safari Mali
UJUMBE wa viongozi wa Afrika Magharibi umeachana na mpango wake wa kwenda Mali kujadiliana na viongozi wa mapinduzi ya wiki iliyopita. Taarifa zinasema kwa sasa viongozi hao wataendesha mazungumzo hayo mjini Abidjan. Taarifa zaidi zinasema uamuzi huo umekuja baada ya maandamano ya watu wanaounga mkono mapinduzi kuvamia uwanja wa ndege katika eneo la kupaa na kutua ndege ili kupinga ujio …
Mali yasimamishwa uanachama
JUMUIYA ya Afrika Magharibi ECOWAS imesimamisha uanachama wa Mali kuafuatia hatua ya jeshi kuoindua serikali ya Rais Amadou Toumani Toure. Viongozi wa Jumuiya hiyo walifikia uamuzi huo katika mkutano uliofanyika nchini Ivory Coast. Sasa viongozi hao kutoka nchi sita wanachama wa ECOWAS wamepanga kusafiri hadi mjini Bamako Mali ili kukutana na baraza kuu la jeshi linalotawala nchi hiyo. Akihutubia waandishi …
Papa Benedict 16 awasili nchini Mexico
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Benedict 16, amewasili nchini Mexico huku akilakiwa na mamia ya waumini waliojipanga kwa kiasi cha umbali wa kilometa 20 katika njia aliyopitia katika Mji Mkuu wa nchi hiyo. Waumini hao walikuwa wakiimba nyimbo za kumkaribisha papa Benedict huku wakisema, Benedict, kaka, sasa wewe ni Mmexico. Wengi wanafikiri makaribisho hayo mazuri, yakisindikizwa na muziki wa …
Dunia yalaani mapinduzi Mali
MATAIFA mbalimbali duniani yamelalamikia kitendo cha wanajeshi wa Mali kufanya uamuzi wa kuipindua Serikali ya Rais Amadou Toumani Toure. Taarikutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) limetaka utawala wa kikatiba kurejeshwa nchini humo mara moja, huku Benki ya Dunia pamoja na Benki ya Maendeleo barani Afrika wakisema wanasitisha baadhi ya shughuli nchini humo. Msemaji wa wanajeshi waasi nchini …
Mshukiwa wa mauaji ya Ufaransa ‘kujisalimisha’
POLISI wenye silaha nzito, wakiwa wamevalia nguo za kujikinga na risasi, wameivamia nyumba moja katika kiunga kilicho kilomita chache kutoka skuli ya Kiyahudi ya Ozar Hatorah, ambako mauaji ya Jumatatu yalitokea. Mashahidi wameliambia shirika la habari la Reuters kwamba walisikia milio kadhaa ya risasi mwendo wa saa 10 na dakika 40 alfajiri kwa saa za Ulaya ya Kati, sawa na …