Wanachama wa GEPF kulipa michango Kupitia Airtel money

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na mfuko wa mafao ya uzeeni kwa watumishi wa serikalini, (GEPF) imezindua huduma itayowawezesha wanachama wa mfuko wa GEPF walioko Tanzania nzima kurejesha na kulipa michango yao ya kila mwenzi kwa kupitia huduma ya Airtel money , Uzinduzi wa makubaliano haya yamefanyika katika hotel ya Gold Crest Mkoani Mwanza na kuhudhuria …

Mama salma Kikwete awatembelea wagonjwa wa kansa-Brasilia

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa amembeba mtoto Anna Julia Telles mwenye umri wa miezi mitatu anayepata matibabu ya kansa katika Hospitali ya watoto wanaougua ugonjwa huo iliyopo mjini Brasilia nchini Brazili. Hospitali hiyo inatoa dawa aina ya chemotherapy kwa wagonjwa ambao ni watoto 500 kwa mwezi na inatibu asilimia sabini ya kansa. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete …

Jumla ya Shilingi bilioni 71 zatumika kununua karafuu Unguja na Pemba,

Na mwandishi wetu RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametoa wito kwa wananchi wa Zanzibar hasa wakulima wa zao la karafuu kutoweka fedha zao majumbani na badala yake waweke kwenye mabenki yaliopo nchini kwa ajili ya usalama wa fedha zao. Dk. Shein aliyasema hayo mara baada ya kutoa zawadi ya vyeti maalum kwa …

TANZANIA yajivunia hatua iliyopiga katika OPG

Serikali ya Tanzania imepiga hatua kubwa katika kutekeleza mpango wa ubia wa uwazi serikalini (Open Government Partnership-OPG) kama ilivyoahidi katika kikao kilichopita Disemba 2011. Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameeleza hatua zilizofikiwa katika kikao hicho cha kwanza cha viongozi wa juu kinachofanyika Brasilia, Brazil. pia, Rais Kikwete pamoja na viongozi wengine kutoka Marekani, Georgia na mwenyeji Brazil wametoa hotuba za ufunguzi. …

MABADILIKO YA TABIA NCHI YAWATISHIA WAKAZI WA KILIMANJARO

Na Mwandishi wetu. WAKULIMA mkoani Kilimanjaro wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuzuia usafirishaji mazao ya nafaka kwenda nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kuongeza nguvu katika kudhibiti matumizi ya nafaka kutengenezea pombe hatua ambayo itasaidia kuwepo kwa chakula cha kutosha nchini na kupunguza tatizo la njaa ambalo limeanza kuwakabili baadhi ya wananchi mkoani humo. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na …

Taliban wavunja gereza Pakistan, wafungwa watoroka

WAPIGANAJI wa Taliban wameshambulia gereza Kaskazini Magharibi mwa Pakistan, na kuwaachilia huru wafungwa karibu 400. Polisi wanasema washambuliaji walitumia bunduki na maguruneti katika shambulio hilo jana usiku huko mjini Bannu, karibu na mpaka wa Afghanistan. Hata hivyo viongozi wa juu wanasema kuwa kati ya wafungwa waliotoroka baada ya kuvunjwa kwa gereza hilo ni wapiganaji na wahalifu wakubwa. Na kati ya …