Sudan yashambulia kusini

Sudan Kusini imeishutumu Kaskazini kuwa imeshambulia kwa mabomu kituo muhimu cha mafuta, ambayo inaonesha mzozo baina ya nchi mbili hizo bado haukumalizika. Juma lilopita, wanajeshi wa Sudan Kusini waliteka visima muhimu vya mafuta vya Sudan kaskazini, huko Heglig, na kuzusha malalamiko ya kimataifa na msukosuko mkubwa. Na picha za satalaiti ya Marekani zinaonesha kuwa sehemu muhimu ya miundo mbinu kwenye …

Iran yaunda ndege isiyohitaji rubani

Iran imeanza kuunda ndege ya ujasusi sawa na ile ya aina ya Sentinel ya Marekani, ambayo ilianguka nchini Iran mwaka jana. Wakuu wa Iran wanasema wamepata maelezo kuhusu namna ndege hiyo inavofanya kazi, kwa kufumbua fumbo la software yake; na sasa inaelewa kikamilifu muundo wa ndege hiyo. Kuna wasiwasi kuwa Iran huenda ikaweza kuigiza rangi maalumu ambayo inasaidia kufanya ndege …

Mradi wa tangi la maji wakamilika-Ziwani Pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa Tangi la Maji la Ziwani Wilaya ya Chake chake Pemba, akiwa katika ziara ya kutembelea miradi mbali mbali ya kijamii ya Mkoa wa Kusini Pemba jana.[Picha na Ramadhan Othman,Pemba.] Pichani ni Tangi la Maji safi na Salama lililojengwa katika shehia ya ziwani wilaya ya Chake …

Dk Shein azungumza na kikosi kazi kilichoshughulikia zao la karafuu

Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi wa Vikosi vya Ulinzi ambao ni Wajumbe wa Kikosi cha (Task Force), ya Taifa kuhusu uvunaji wa zao la karafuu,alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kusini Pemba jana.[Picha na Ramadhan Othman,Pemba.] Naibu Waziri wa …

JAJI CHANDE AHIMIZA MABADILIKO KATIKA MAHAKAMA ZA AFRIKA MASHARIKI

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande amezitaka mahakama katika nchi wanachama wa Afrika Mashariki kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo wake wa utendaji ili kuleta ufanisi na maamuzi ya haki kwa wakati kwa wananchi wa kanda hiyo. Alisema hatua hiyo itarejesha imani na matumaini kwa mahakama katika nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na kuacha ugoigoi katika kushughulikia mabadiliko …

Rais wa Zanzibar Dr. Shein asisitiza umuhimu wa kilimo cha kisasa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Maliasili Afani Othman Maalim,alipokagua ujenzi wa Mtaro katika matayarisho ya kilimo cha Mpunga wa umwagiliaji huko Makombeni Mkoani Pemba.[Picha na Ramadhan Othman Pemba.] Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Juma Kassim Tindwa,akitoa Taarifa ya Mkoa wake kwa Rais wa …