Marekani imeandaa azimio ambalo limelenga kuidhinisha vikwazo dhidi ya serikali za Sudan na Sudan kusini ikiwa hazitasitisha mapigano mara moja na kurejea kwenye mazungumzo ya amani. Azimio hilo linaunga mkono pendekezo la Umoja wa Afrika mapema wiki hii. Muungano wa Afrika umezitaka Sudan na Sudan Kusini kutekeleza mkataba wa amani kwa muundo mpya wa AU. Azimio hilo linazingatia sana onyo …
AU yazitaka Sudan na Sudan kusini kutekeleza muundo wa amani
Muungano wa Afrika umezitaka Sudan na Sudan Kusini kutekeleza mkataba wa amani kwa muundo mpya wa AU. Kamishna wa baraza la usalama wa AU, Ramtane Lamamra amesema muungano huo utachukua hatua zinazostahili iwapo mojawapo ya nchi hizo itashindwa kutekeleza mpango wa amani uliopendekezwa katika muda uliopangwa. Baada ya kuwa kimya kwa muda, hatimae sauti ya Afrika inasikika kufuatia mzozo huo …
Charles Taylor kuhukumiwa leo
MAJAJI katika Mahakama maalum ya vita nchini Sierra Leone, leo watatoa hukumu dhidi ya aliyekuwa Rais wa Liberia Charles Taylor kwa kuhusika na vita hivyo vilivyodumu kwa miaka 10. Taylor anakabiliwa na mashtaka 11 ikiwemo ubakaji na mauaji ya raia wa Sierra Leone. Ikiwa atapatikana na hatia atakuwa rais mstaafu wa kwanza kuhukumiwa na Mahakama ya kimataifa. pia kiongozi huyo …
Bingu wa Mutharika azikwa nyumbani
RAIS wa zamani nchini Malawi, Bingu wa Mutharika, amezikwa nyumbani kwake kusini mwa nchi. Wa Mutharika alifariki dunia mwezi jana baada ya kupatwa na mshutuko wa moyo. Marehemu alizikwa kando ya kaburi la mkewe Ethel Mutharika. Maelfu ya waombolezaji wakiwemo marais kadhaa barani Afrika walihudhuria maziko hayo yaliyokuwa ya kitaifa. Rais Mpya Joyce Banda aliwaongoza waandamanaji ambapo alitetea baadhi ya …
Waandamana nusu uchi kulalamikia Polisi
KUNDI la wanawake wamevua nguo, nusu uchi kulalamikia kitendo cha Polisi wa Uganda anayedaiwa kumdhalilisha kingono mwanasiasa wa upinzani. Kanda ya video imeonesha Polisi akimtomasa tomasa matiti Bi. Ingrid Turinawe wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) baada ya kumkamata kuzuia maandamano ya wiki iliyopita. Tayari Naibu Kamishina wa Polisi nchini Uganda, Andrew Kaweesa ameomba radhi na …
Katibu Mkuu wa UN akemea hatua ya Sudan
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bani Ki Moon amelaani vikali mashambulio ya ndege za Sudan Kwenye mpaka wake na Sudan Kusini. Bw Ban amesema hali hii inachochea zaidi uhasama kati ya nchi hizo mbili. Katibu mkuu huyo ametaka Sudan isitishe mashambulio mara moja akiongeza kuwa harakati za kijeshi kamwe haziwezi kusuluhisha mzozo wa mipaka kati ya nchi hizo mbili. …