KIONGOZI wa mapinduzi yaliyofanywa mwezi uliopita nchini Mali, Kepteni Amadou Sanogo, amekataa uamuzi wa Jumuia ya Afrika Magharibi, ECOWAS, kutuma wanajeshi nchini humo. Alisema jeshi – ambalo rasmi limekabidhi madaraka kwa serikali ya mpito – halikushauriwa juu ya uamuzi uliofikiwa na viongozi wa nchi za ECOWAS siku ya Alkhamisi huko Ivory Coast. Wanajeshi wa Mali walifanya rabsha kwenye mkutano baina …
Mashariki mwa Congo khali si shwari
Ripoti kutoka mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo zinasema kuwa mapigano makali yametokea baina ya jeshi la serikali na askari watiifu kwa jenerali aliyeasi, Bosco Ntaganda. Inaarifiwa kuwa maelfu ya watu wamelikimbia eneo hilo katika majuma ya karibuni, tangu askari mia kadha wanaomuunga mkono Jenerali Ntaganda kuasi jeshini. Mwandishi wa BBC mjini Kinshasa anasema, mvutano unaozidi mashariki mwa Congo …
Waziri wa zamani wa Libya afariki Dunia
WAZIRI wa mafuta wa zamani wa Libya amekutikana amekufa katika mji mkuu wa Austria, Vienna, karibu na mto Danube, kwa mujibu wa Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje ya Austria. Shukri Ghanem, aliyekuwa na umri wa miaka 69, alikuwa mmoja kati ya wakuu maarufu waliokimbia kutoka serikali ya Kanali Gaddafi wakati wa ghasia za Libya. Hakujatolewa maelezo zaidi, lakini …
Rais wa Malawi amfuta kazi hasimu wake
Rais mpya wa Malawi Joyce Banda amemfuta kazi Waziri wa mambo ya nje Peter Mutharika, kakake Marehemu Rais Bingu Wa Mutharika aliyefariki dunia mwezi huu. Mutharika alitarajiwa kurithi Marehemu Kakake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2014 ambapo Bingu Wa Mutharika alitarajiwa kustaafu. Mabadiliko ya baraza la mawaziri yametokea siku chache baada ya maziko ya Rais huyo mapema wiki hii. Bi. …
ECOWAS kutuma Jeshi Mali na G.Bissau
Viongozi wa kanda ya Afrika Magharibi wameafikiana kutuma wanajeshi katika nchi za Mali na Guinea-Bissau kufuatia mapinduzi katika hizo. Nchi wanachama wa ECOWAS zilitoa taarifa ya pamoja baada ya kufanya kikao cha dharura ambapo wanajeshi kati ya 500 na 600 watatumwa Guinea-Bissau. Wanajeshi wengine 3,000 wataelekea Mali kusaidia kipindi cha mpito pamoja na kuyakomboa maeneo ya kaskazini ,yanayodhibitiwa na waasi …
Mahakama yamtia hatiani Charles Taylor
MAJAJI katika Mahakama maalum ya kimataifa wamempata na hatia Rais wa zamani nchini Liberia Charles Taylor na hatia ya kufadhili vita nchini Sierra Leone. Taylor ameshtakiwa mbele ya mahakama maalum inayochunguza uhalifu wa kibinadamu nchini Sierra Leone. Kesi dhidi ya kiongozi huyu imechukua takriban miaka mitano. Taylor alituhumiwa kwa kuwaunga mkono waasi ambao waliwaua maelfu ya raia katika vita vya …