MAREKANI imetibua njama ya kundi la kigaidi la al-Qaeda katika ufuo wa Arabia ya kulipua bomu sawa na alililokuwa nalo mtu aliyejaribu kulipua ndege ya shirika moja la Marekani iliyokuwa ikitoka Yemen kuelekea Marekani mwaka 2009. Hata hivyo majasusi wanasema bomu lililopatikana lilikuwa la hali ya juu kuliko lile la mwaka 2009. Maafisa wanasema jaribio hilo lilikuwa limepangwa na kundi …
Kwacha yashuka thamani kwa 50%
WATU nchini Malawi, wamekuwa wakikimbilia kununua bidhaa muhimu , kufuatia hofu ya kupanda kwa bei ya chakula baada ya benki kuu kushusha thamani ya sarafu ya nchi hiyo ‘kwacha’ kwa 50%. Mwandishi wa BBC mjini Blantyre, Raphael Tenthani anasema kuwa maduka mengi yalikuwa hayana bidhaa kama sukari, mafuta ya kupikia na mkate. Thamani ya kwacha, ilishushwa kama sehemu ya mpango …
Jeshi lasitisha mapigano DRC
JESHI limetangaza kusitisha mapigano na kuwapa waasi hadi siku ya Jumatano kujisalimisha. Jeshi nchini DRC linasema limedhibiti eneo zima la Masisi kutoka kwa waasi watiifu kwa kiongozi wa waasi Bosco Ntaganda. Maelfu ya watu wametoroka makwao katika eneo hilo baada ya wiki nyingi za mapigano. Generali Ntaganda, ambaye anajulikana kwa jina lengine kama “The Terminator”, anatakiwa na mahakama ya kimataifa …
Wanamgambo wawauwa 17 Pakistan
Watu wasiopungua 17 wameuawa katika mashambulio ya mabomu ya kujitoa mhanga nchini Paskitan, katika mji mmoja karibu na mpaka wa nchi hiyo na Afganistan. Maafisa wa serikali ya Pakistan, wamesema mshambuliaji huyo wa kujitoa mhanga alifika hapo kwa miguu na kujilipua karibu na kizuizi cha polisi katika eneo linalokaliwa na watu wa kabila la Bajur. Wapiganaji wa Taliban wamekiri kutekeleza …
Charles Taylor miaka 8 Jela.
Waendesha mashtaka katika kesi ya rais wa zamani wa Liberia Charles Charles Taylor, wameomba adhabu ya kifungo cha miaka 8 jela itolewe dhidi yake. Bw Taylor alipatikana na hatia ya makosa ya uhalifu wa kivita katika mahakama ya kimataifa mjini The Hague, wiki iliyopita. Katika pendekezo lao lililowasilishwa mbele ya mahakama hiyo maalum inayosikiza kesi ya Seirra Leone, waedesha mashtaka …
Sudan kusitisha Uhasama baina ya Kusini
Jamhuri ya Sudan imekubaliana na mpango wa Muungano wa Afrika (AU) wa kusitisha uhasama na Sudan Kusini, lakini imesema itajilinda iwapo itashambuliwa. Jumatano iliyopita, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, lilizipa nchi hizo mbili hadi Ijumaa kusitisha mapigano, la sivyo ziwekewe vikwazo. Lakini kumekuwa na ripoti za kuongezeka kwa mapigano. Sudan Kusini ilisema siku ya Alhamisi kuwa ndege za …