Kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya Uhalifu ICC Luis Moreno Ocampo ametoa ombi la kukamatwa kwa kiongozi wa kundi la wanamgambo wa kihutu la FDLR katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Sylvestre Mudachumura. Bosco Ntaganda aongezewa mashitaka na Ocampo Bwana Ocampo pia anataka mashtaka mapya kufunguliwa dhidi ya Jenerali Muasi wa jeshi la Jamhuri …
majadiliano ya amani yazidi kuzorota- Afghanistan
Watu wenye silaha wamempiga risasi na kumuua mjumbe wa ngazi ya juu wa majadiliano ya amani na kiongozi wa zamani wa Taliban mjini Kabul jana Jumapili, katika pigo jingine katika juhudi za Afghanistan za kumaliza mapigano yaliyodumu kwa muongo mmoja sasa ya kundi la Taliban. Arsala Rahman , mjumbe wa baraza la juu la amani aliuwawa katika tukio la kushambuliwa …
Kamanda wa LRA akamatwa
Jeshi la Uganda linasema kuwa limemkamata afisa mwandamizi wa kundi la wapiganaji la LRA – kundi ambalo limekuwa likiwauwa na kuwateka nyara watu Afrika mashariki na ya kati, kwa zaidi ya miaka 20. Kiongozi wa LRA, Joseph Kony anasakwa na Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, kwa uhalifu wa vitani. Washauri wa Marekani wamekuwa wakisaidia majeshi ya nchi za Afrika mashariki …
Ugiriki haijapata Serikali
HADI sasa Ugiriki haijaweza kupata Serikali na hatima ya nchi hiyo ndani ya sarafu ya euro sasa imo mashakani, baada ya chama cha mrengo wa kushoto kutangaza kushindwa kufikia makubaliano ya kuunda Serikali. Mpira sasa uko upande wa kiongozi wa chama cha kisoshalisti cha PASOK, Evangelos Venizelos, anayekabiliwa na jukumu lisilo shukurani la kuunda serikali hivi leo, kufuatia kushindwa kwa …
Obama aunga mkono ndoa za jinsia moja
RAIS wa Marekani, Barack Obama, ameunga mkono ndoa za jinsia moja, huku maamuzi hayo yakibadilisha msimamo wake wa awali. “Nimefanya maamuzi ya kimapinduzi na lazima Wamerikani wote watendewe sawa.” Alisema Rais Obama kwa upole katika sentensi yake ya Kwanza kutoka kinywani kwa Rais huyo wa Marekani wakati akifanya mahojiano na Televisheni ya ABC nchini Marekani na kukubali ndoa hizo. Huku …
Maafisa wa Zimbabwe kuchunguzwa
Afrika Kusini ni sharti ichunguze maafisa wa Zimbabwe wanaodaiwa kuhusika na tuhuma za mateso dhidi ya wanasiasa wa upinzani mwaka 2007, kulingana na uamuzi wa mahakama kuu nchini Afrika Kusini. Jaji wa mahakama hiyo amesema kuwa chini ya sheria za kimataifa Afrika kusini ina jukumu la kuchunguza tuhuma za ukiukwaji wa haki za kibinadamau. Awali Viongozi wa mashtaka walikataa kuchunguza …