Taylor “Mashahidi walinunuliwa”

RAIS wa zamani wa Liberia Charles Taylor anayetuhumiwa kwa makosa ya kivita amewashambulia waendesha mashtaka kuwa waliwalipa mashahidi wa upande wa mashtaka ili wamkandamize. Taylor ambaye alikutwa na hatia mwezi uliopita alisema hayo wakati akitoa maelezo kwenye mahakama ya Kimataifa ya makosa ya Jinai ya The Hague. Hiyo ni nafasi yake ya mwisho ya kujieleza katika mahakama hiyo kabla ya …

Zaidi ya watu bilioni 4.7 wanakabiliwa na njaa Sudan kusini

ZAIDI ya nusu ya raia wa Sudan Kusini wanakabiliwa na baa la njaa. Shirika la chakula duniani limesema kuwa hali hiyo imechangiwa sana na machafuko kati ya Sudan Kusini na jirani zao Sudan. Shirika hilo limesema kuwa mapigano katika maeneo ya mipaka na pia kufungwa kwa visima kadhaa vya mafuta kumetatiza uchumi wa Sudan Kusini. Ripoti hiyo inaonya kuwa kadiri …

Pakistan kuifungua tena njia ya misafara ya NATO

WAZIRI wa Mambo ya Nchi za Nje wa Pakistan amesema wakati umewadia kufungua njia ya misafara ya NATO kuelekea Afghanistan, akisema Serikali imetoa ujumbe unaoeleweka kwa kuifunga njia hiyo, ikilipiza kisasi kwa mashambulizi ya Marekani yaliyouwa wanajeshi wa Pakistan. Kauli ya waziri huyo, Hina Rabbani Khar, inaonesha kuwa shinikizo la Marekani dhidi ya Pakistan limefanikiwa, ingawa hadi sasa Marekani imakataa …

IAEA kukagua Kituo cha Kijeshi cha Iran

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Kudhibiti Matumizi ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) limesema litaishinikiza Iran iwaruhusu wakaguzi kuingia kwenye kituo chake cha kijeshi, ambacho kinashukiwa kuwa na chumba maalum cha majaribio ya miripuko mikubwa ambayo inaweza kutumiwa kuunda silaha za nyuklia. Iran ambayo imekana shutuma za nchi za magharibi kwamba inajaribu kuunda bomu la Atomiki, imekataa kuwaruhusu wakaguzi wa …

Wafungwa wa Kipalestina waongeza masharti

WAFUNGWA wa Kipalestina walio katika mgomo wa kutokula wameongeza masharti zaidi ili kusitisha mgomo wao unaowahusisha wafungwa 1,550 na mahabusi wawili unaoendelea kwa siku ya 76 sasa. . Wafungwa na mahabusu hao wameutaka utawala wa Israel uregeze masharti kwa kuruhusu ndugu zao wawatembelee gerezani, ruhusa ya kupata elimu, kuondolewa kwa utaribu wa kumuweka mtu kizuizini bila ya kufunguliwa mashitaka. Kukiwa …

Shehena ya silaha yanaswa DRC

SHEHENA silaha imenaswa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika shamba linalomilikiwa na mbabe wa kivita wa zamani Jenerali Bosco Ntaganda. Kwa mujibu wa jeshi, silaha nyingine zimenaswa katika maeneo mengine mawili katika Mkoa wa Kivu ya Kaskazini, eneo ambalo lilikumbwa na mapigano kati ya wanajeshi na waasi. Inadaiwa silaha hizo zilikuwa za wapiganaji watiifu kwa Jenerali muasi Bosco …