RAIS wa Misri wanajianda kushiriki katika uchaguzi wa kwanza huru tangu mapinduzi ya kiraia yaliomuondoa Rais Hosni Mubarak mamlakani miezi 15 iliopita. Watu milioni 50 wanashiriki kwenye uchaguzi huo Wapiga kura milioni 50 watashiriki katika uchaguzi huu ambao usalama unapewa kipa umbele. Baraza kuu la jeshi nchini humo ambalo lilichukuwa utawala baada ya mapinduzi ya kiraia mwezi wa Februari mwaka …
Nato kukabidhi jukumu la ulinzi Afghanstan 2013
JUMUIYA ya kujihami ya NATO imesema kuwa itakabidhi jukumu la ulinzi wa Afghanistan kwa nchi hiyo katikati ya 2013 pamoja na kutangaza kuanza mfumo wake mpya wa kinga ya makombora barani Ulaya utakaokamilika 2020. Kutangazwa kwa hatua hiyo kumezusha hali ya kutoelewana baina ya NATO na Urusi ambayo imeendelea kusisitiza ipatiwe uhakika wa kisheria unaothibitisha kuwa mpango huo hauilengi nchi …
Polisi “kazi ipo Kesi ya Terre’blanche leo”
POLISI wameimarisha doria katika mji wa Ventersdorp, nchini Afrika Kusini ambapo mahakama inasubiriwa kutoa hukumu kwa vijana wawili wa Kiafrika wanaotuhumiwa kumuua Eugene Terre’ Blanche miaka miwili iliyopita. Bwana Terre’ blance alikuwa kiongozi wa mrengo wa kulia wa vuguvugu la kupigania utawala wa kizungu la Afrikaan Resistance Movement. Wanaharakati wengi wa kutoka vuguvugu hilo hii leo wanatarajiwa kupiga kambi nje …
Malawi kubatilisha sheria ya mapenzi
RAIS wa Malawi,Joyce Banda amesema kuwa anataka nchi hiyo ibatilishe sheria inayoharamisha ndoa za jinsia moja na kuifanya nchi ya kwanza ya kiafrika kufanya hivyo tangu mwaka 1994. Wananume wawili raia wa nchi hiyo walihukumiwa kifungo cha miaka 14 gerezani mwaka 2010 baada ya kutangaza kuwa wanataka kuoana. Baadhi ya viongozi wa nchi za magharibi, hivi karibuni wametishia kusitisha msaada …
Wangaalizi wa amani hatarini nchini Syria
WAANGALIZI wa Umoja wa Mataifa nchini Syria wameondolewa katika mji wa Khan Sheikhoun, kaskazini mwa nchi hiyo siku moja baada ya msafara wao kupigwa na kombora katika makabiliano kati ya vikosi vya serikali na waasi. Mashambulizi hayo ambayo yalikuja muda mfupi baada ya shahidi mmoja kusema kuwa majeshi ya serikali ya Syria yaliwauwa kwa risasi waombolezaji waliyokuwa kwenye msiba karibu …
Watoto 150 wajumuishwa Jeshini-DRC
JENERALI aliyehasi jeshini, Bosco Ntaganda ambae anasakwa na Mahakama ya Kimatiafa ya Jinai -ICC bado anadaiwa kuingiza idadi kubwa ya watoto katika jeshi lake. Shirika la Human Rights Watch (HRW) linasema kuwa katika mwezi uliopita watoto wapatao 150 wa kike na wakiume wamejumuisha jeshini. Watoto hao wote wanatoka katika eno la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Wale ambao …